Naibu Meya wa Wialaya ya Kinondoni Rwegasira Samson akiangalia kura zikihesabiwa mara baada ya kupigiwa na Madiwani wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salam Agosti 26, 2022.
Na Mwandishi Wetu
DIWANI wa Kata ya Makongo Jimbo la Kawe Rwegasira Joseph Samson ameshinda kwa kura asilimia 100 za kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni.
Kura hizo zilipigwa na Madiwani 25 jana jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Manispaa ambapo Rwegasira alipata kura za ndio za madiwani wote.
Akizungumza kabla na baada ya ushindi huo Naibu Rwegasira, alisema kuwa anaahidi ushirikiano kwa hali na mali na Meya wa Manispaa hiyo Songoro Mnyonge.
"Kwanza nipende kuwashukuru viongozi wote wa Manispaa akiwemo Mkurugenzi, Meya, Naibu Meya aliyemaliza muda wake Mhe. Heri Missinga maalufu kama 'Obama' pamoja na madiwani wote walionipigia kura zote za ndio, alisema Naibu Meya mpya, na kuongeza;
"Ninachotaka kuwaahidi ni kwamba nitashirikiana na viongozi wangu katika kuhakikisha Manispaa yetu inakuwa salama na niwatoe hofu kwamba nitaendelea kumshauri Meya kwani ndiye Bosi wangu."
Aidha, alisema Rais Samia Suluhu Hassan anafanya juhudi kubwa za kuwaletea maendeleo wananchi hivyo yeye atashirikiana vyema na viongozi wake kuhakikisha juhudi za Rais zinaendelea kusonga mbele.
"Mhe. Rais anajitahidi sana kutuhidhinishia fedha nyingi za miradi mbalimbali ikiwemo mashule, masoko, na miradi mbalimbali ya maendeleo hiyo nitaendelea kushirikiana na viongozi wangu kuhakikisha inatekelezwa,"alisema Naibu Meya Rwegasira.
Alisema anamtoa hofu Meya Mnyonge kwamba atakuwa mshauri wake mzuri na atashirikiana naye kwa asilimia 100.
Meya Songoro Mnyonge alimpongeza Naibu Mpya Rwegasira kwa kuibuka kidedea kwa ushindi wa asilimia 100 na pia alimpongeza Naibu Meya Obama kwa uvumilivu wake wa kufanya kazi kwa moyo mkunjufu.
Obama alisema kazi ya unaibu pia inachangamoto zake hivyo lazima uwe mvumilivu.
Mwenyekiti wa muda wa uchaguzi ambaye pia ni Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Kinondoni Stella Msophe alimpongeza Meya mpya Rwegasira pamoja na madiwani wote waliopiga kura na kusema kuwa wamefanya uteuzi uliokamilika kwa kutoaribu kura hata moja.
Baadhi ya Madiwani wa Wilaya ya Kinondoni wakiwa katika kikao na kumpigia kura Naibu Meya Rwegasira Samason jijini Dar es Salaam Agosti 26,2027.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...