Wanakijiji wa Kijiji cha Ruhita, Wilaya ya Kasulu Mjini wamefurahishwa na kutatuliwa kwa kero yao ya muda mrefu ya kukosa maji, ambapo kwa sasa mradi wa maji umekamilika kutokana na jitihada zilizofanywa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.
Akiongea leo tarehe 04 Agosti 2022, wakati wa kukagua shughuli za maendeleo katika Kata ya Ruhita, ameeleza kuwa yeye kama Mbunge wa jimbo hilo anaendelea kuhakikisha mipango ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kusogeza karibu kwa wananchi huduma muhimu za kijamii inatekelezwa, ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za maemdeleo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wanakijiji wa Ruhita wamemshukuru Mbunge huyo kwa jitihada zake za kuhakikisha anawaletea huduma za kijamii karibu ikiwemo huduma ya maji ambayo wameeleza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa na kilio hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...