Picha ya pamoja za Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene pamoja  makundi mbalimbali mara baada ya kuzindua Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai inayofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.


*Viongozi wa Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai kwenda na mafundisho ya ndoa katika mkazo

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera , Bunge na Uratibu George Simbachawene amesema kuwa kwa kipindi cha miezi tisa kwa eneo moja la Wilaya ya Temeke Ndoa 350 zimevunjika.

Simbachawene ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni linalofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Simbachawene amesema viongozi wa dini wana kazi ya kufanya kutokana na mmomyoko wa maadili ambapo unachangia ndoa nyingi kuvunjika na kuwa na familia zinazolelewa na upande mmoja tu.

Amesema hali ndoa kuvunjika sio hali nzuri kwani takwimu hiyo ni Manispaa moja ya Temeke na hajajua hali ya nchi nzima ikoje ambapo viongozi wa dini wana kazi ya kufanya katika eneo la kujenga familia.

"Ndoa hizo zinafungwa na sherehe kubwa na kujipamba lakini hizo zinavunjika na viongozi wa dini wakiwa wanaziongoza kwa baraka naomba sasa viongozi wangu mkaliangalie hili katika kufundisha kwa ndo kuvunjika ni chukizo la Mungu"amesema Simbachawene.

Aidha amesema kuwa hata maendeleo yanafanywa na serikali haitakuwa ya maana kama familia zetu hazijengwa katika misingi ya uadilifu wa kuweza kusimamia maendeleo hayo.

Waziri Simbachawene amesema kuwa somo la ndoa liwe sehemu ya kambi hiyo kwani kuna vijana walioko katika ndoa na wengine wanatarajia kuingia na hao walio katika kambi wasiwe sehemu ya ndoa za kuvunjika.

Hata hivyo Waziri Simbachawene ametaka waumini hao kushiriki Sensa kikamilifu .

Nae Askofu wa Jimbo la Mashariki Kati Mwa Tanzania Joseph Mngwabi amesema kuwa katika masuala yote katika kambo sehemu ya ndoa litakuwa la kipekee kwa kulifundisha kwa kufuata maandiko ya Mungu.

Amesema kuwa katika kipindi cha elimu juu ya sensa wamelipokea na watashiriki waumini wao katika kuendelea kuunga mkoa serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Hassan Suluhu.

Mchungaji wa Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai Methusela Masunga amesema kambi hiyo ni ya siku saba ambapo watafanya suala ibada pamoja ba kutoa huduma kwenye jamii.

Amesema Kanisa la Sabato Magomeni wako pamoja na Serikali kuendelea kuunga mkono kwa kila jitihada zinazofanyika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene akizingumza wakati wa Uzinduzi wa Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai inayofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Askofu wa Jimbo la Mashariki Kati Mwa Tanzania Joseph Mngwabi akitoa maelezo kuhusiana na kambi pamoja na shughuli za kambi wakati uzinduzi uliofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Mchungaji wa Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai Methusela Masunga akizungumza kuhusiana na waliojipanga katika kwenda na kambi hiyo katika maombi na kuilishilisha neno la Mungu , jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene akipanda mti mara baada  ya kuzindua  Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai inayofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene akipokea vitabu kutoka kwa  viongozi wa Dini wa Kanisa la Sabato mara baada  kuzindua Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai inayofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.



Picha za pamoja za Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene pamoja  makundi mbalimbali mara baada ya kuzindua Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai inayofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Waumini wakimsikiliza Waziri Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene  hayupo picha wakati wa uzinduzi wa  Kambi ya Kanisa la Sabato Magomeni Mwembechai inayofanyika Kwembe Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...