

*Huduma za Bima na elimu kuhusu bima zinapatikana
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mbeya
SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) linawahamasisha wananchi kutembelea maonesho ya Nane Nane Kitaifa Kanda ya Mbeya kupata elimu ya huduma za bima katika maonesho hayo.
Katika kupata elimu bima hiyo pia wananchi wanaweza kukata bima mbalimbali na kupata ndani ya muda mfupi.
Akizungumza na Michuzi Blog ndani ya Maonesho ya Kilimo Kitaifa Kanda Mbeya Nane Nane Meneja wa NIC Kanda ya Mbeya Justine Iseni amesema wamejipanga kutoa huduma ndani ya maonesho hayo.
Iseni amesema kuwa huduma zote za bima zimesogezwa katika Maonesho ya Nane Nane
Amesema NIC imejipanga kuwafikia wadau wote wakiwemo wakulima na wafugaji kupata bima ambapo kilio cha wananchi kitakuwa kimeisha.
Amesema kuwa NIC imekuwa na mifumo ya tehama rahisi na kufanya mtu kujisajili na kuweza kupata bima moja kwa moja.
Aidha amesema kazi inaendelea lakini kazi hizo lazima tuliochini tuhakikishe tunatoa huduma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...