

KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Dkt.Mwinyi Talib Haji na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe. Dkt.Khalid Salum Mohammed, wakifuatilia utiaji wa Saini ya ujenzi wa Barabara za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja zaidi ya kilomita Mia Moja, zitakazojengwa na Kampuni ya CCECC kutoka Nchini China, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar

WAKUU wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza baada ya utiaji wa Saini ya Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja zaidi ya Kilomita Mia Moja, zitakazojengwa na Kampuni ya CCECC kutoka Nchini China, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishuhudia utiaji wa Saini ya Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Juu (Flyover) katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, kwa upande wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar amesaini Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Bi.Khadija Khamis Rajab na kwa upande wa Kampuni ya CCECC kutoka China amesaini Mkurugenzi Muendeshaji Bw. Zhang Junle Le, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar

BAADHI ya Mawaziri na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatilia Utiaji wa Saini ya Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Juu (Flyover) katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza baada ya utiaji wa saini , hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza baada ya utiaji wa Saini ya Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Juu (Flyover) katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar amesaini Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Bi. Khadija Khamis Rajab na kwa Kampuni ya CCECC amasaini Mkurugenzi Muendeshaji Bw. Zhang Junle Le, hafla hiyo imefanyika leo 6-8-2022, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...