
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imezuia kukata na kupandisha hadhi maeneo ya utawala kwa sababu yanaongeza gharama kwa Serikali.
Rais Samia amesema hayo leo wakati akihutubia wananchi wa Njombe katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba.
Aidha, Rais Samia amesema mwelekeo wa Serikali ni kunyanyua hali ya uchumi wa nchi ili kuinua hali ya maisha ya mwananchi mmoja mmoja.
Rais Samia pia ametoa wito kwa Viongozi nchini kusimamia ipasavyo miradi inayotekelezwa na Serikali ili kuwajengea fursa Watanzania kufanya shughuli za maendeleo na kuinua kipato.
Vile vile, Rais Samia amewataka Viongozi wa Kata, Wilaya na Mikoa kuhudumia wananchi na kutatua kero zao kwa kuzingatia utawala bora.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...