Na Damian Kunambi Njombe

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wakazinwa mkoa wa Njombe kumtumia ipasavyo mkuu wa mkoa mpya Antony Mtaka kwakuwa ameletwa kwaajili ya kufanya kazi.

Rais Samia ameyasema hayo mara baada ya kupokelewa mkoani Njombe akitokea mkoa wa Mbeya na kuongeza kuwa mkuu huyo wa mkoa alikuwa hana kazi ya kufanya pindi alipokuwa mkoani Dodoma hivyo kwakuwa ni kijana mzuri na mchapa akaona ni vyema kumlaeta mkoa wa Njombe.

"Nimewaletea mkuu wa mkoa Antony Mtaka mmemuona? Sasa mkamtumie vizuri maana alipokuwa Dodoma hakuwa na chakufanya bali alkuwa ni mtu wa kutupokea na kutusindikiza sasa huku amekuja kwaajili ya kazi, ninajua ni kijana mzuri sana na atafanya kazi ipasavyo"

Aidha Rais Samia amesema kuwa Katika serikali yake hakuna aliye mtawala bali kuna watoa huduma kulingana na ahadi zilizopo katika ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi hivyo endapo kuna mwananchi atakosa huduma stahiki anapaswa kutoa taarifa.

Amesema viongozi wa serikali hawapaswi kujiona kama ni watala bali watambue kuwa wao ni watoa huduma kwa wananchi na pale watakaposhindwa kutoa huduma stahiki wananchi hao wanapaswa kuyoa taarifa.

Sanjari na hilo pia Waziri wa kilimo Hussen Bashe amewajulisha wakulima wa zao la Parachichi mkoani Njombe kuwa katika msimu ujao wa mavuno kutakuwa na bei elekezi ya zao hilo ili kuhakikiasha mkulima ananufaika moja kwa moja na kufanya kilimo hicho kuwa chenye tija.

Awali mbunge wa jimbo la Wanging'ombe ambaye pia ni naibu waziri wa Tamisemi Festo Dugange aliiomba serikali kuamngalia vyema soko la zao hilo kwani katika msimu huu wakulima walio wengi wamepata hasara kwani wameuza mazao yao hayo kwa sh. 800 kwa kilo badaya ya 2000 ya awali.


Hata hivyo kwa upande wake Waziri wa Uwekezaji, viwanda na biashara Ashatu Kijaji amesema katika mwaka huu wa fedha uliokwisha tani zaidi ya 40,000 za parachichi zimeuzwa nchi za nje jambo ambalo awali halikuwahi kutokea.

Amesema kwa ndani ya wizara yake wameweze kutengeneza mashine za kuchakata zao hilo la parachichi lengo likiwa ni kuhakikisha vijana wazawa wanakuwa na uwezo wa uchakataji licha ya kupatikana wawekezaji.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...