Na Mwandishi Wetu , Michuzi TV- Muheza

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba pamoja na Mbunge wa Jimbo la Muheza katika Mkoa huo Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA wamempongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo.

Wakizungumza mbele ya Katibu MKuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo viongozi hao wamesema wanatoa shukrani hizo za Rais kwa niaba ya Wananchi wote ambao wamekuwa mashuhhuda wa miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika nyanja mbalimbali.

Akizungumza zaidi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema wanashukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza kilio cha wananchi wa milimani ambako tatizo kubwa lilikuwa barabara lakini Rais Samia tayari amesikia kilio hicho na ametoa fedha kwa ajili ya kujenga barabara kwa kiwango cha lami kilometa 10 na tayari ujenzi umeanza.

"Sasa Rais ameongeza kilometa tatu nyingine zijengwe kwa kiwango cha lami,hivyo lami itafika mpaka huko milimani,ndugu Katibu Mkuu naona ulikuwa unauliza maswali mengi kuhusu taarifa tuliyokuwa tunakusomea hapa,kwanza ulikuwa sahihi kutokana na umakini wako, maana yake hukukubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia

"Maana taarifa nilizokuwa nazo alizonipa Mkuu wa Wilaya Halima Bulembo ambaye alikuwa anasimamia hapa kwa niaba ya Serikali,kwa niaba ya Rais kusukuma maendeleo aliniambia nguvu za wananchi walioanza shule hii ilikuwa madarasa mawili na yalishaisha mpaka usawa wa linta, kwa gharama za Serikali maana yake ni Sh milioni 7.5 kwa kila jengo, hivyo kwa majengo mawili ni Sh milioni 15 , Ukiondoa na hizi Sh.milioni 11 maana yake ni zaidi ya Sh milioni 26 au inakaribia milioni 30 hizi ndio nguvu za wananchi

"Wananchi tunatambua mchango wenu mmejitoa na tutaendelea kuweka thamani ,ukiona maswali yako ni ya msingi, shule hii ililetewa fedha kama shule nyingine Tanzania ,zote zilitolewa siku moja , nitawapa mfano nilikotoka huko kulikuwa na Halmashauri moja inaitwa Mbozi ndio ilikuwa Halmashauri ya mwisho kujenga shule kwa kutumia hizi fedha milioni 470 ,wao walianza mwezi wa nne kwasababu walikuwa wakijadiliana wapi waijenge ndio wa mwisho hao lakini leo majengo yote yamekamilika kwa fedha hizo hizo Sh.milioni 470,"amesema.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamisi Mwinjuma amesema pamoja na kuwa na miradi mingi wilayani humo wameamua kumpeleka Katibu Mkuu kwenye hiyo Shule ya Sekondari Kisiwani ilikuwa la kimkakati kabisa kwasababu kwanza itaondoa hadithi ya watoto kutembelea kilometa 23 kwenda shule kupata elimu ya Sekondari lakini pia kuona barabara yao.

"Mimi nilitaka Katibu Mkuu aione kwa macho yake na nawashukuru wananchi kwa jinsi mlivyojitokeza kwa wingi, Katibu MKuu ameona haja ya maendeleo ambayo wananchi wanayo ,hivyo tunamuomba afikishe ujumbe kwa Rais kulingana na changamoto za Kata ya Kisiwani isiwani na namna mnavyotaka zitatuliwe, mradi huu wa shule wakati naingia kuwa Mbunge ungeletwa usingeamini kama kutakuwa n shule.

"Miaka mingi imepita kumekuwa na mapigano mengi yamefanyika lakini imeshindikana, hata nilipopewa nafasi ya kuchagua shule ya milioni 600 ya kwanza iende wapi, mimi ndio nilichagua ije Kata ya Kisiwani , utufikishie salamu kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwafikia Wananchi hao wanyonge kwa kuwapunguzia Watoto kutembea kilometa 23 kwasababu hata lile la kufuta ada kutoka darasa la kwanza mpaka kidato cha Sita lingekuwa haliwasaidii chochote kama wangekuwa wanatembea umbali ule bado.

"Lakini tunachangamoto kadhaa kama ilivyoziona na kubwa ni za kijiografia ya Kata ya Amani na Kisiwani ikiwa ndani yake ni ngumu kweli kweli, nilikuwa natamani mvua ingekuwa imenyesha kidogo ujionee kwa macho yako lakini naamini hii uliyoipata ni trela ni kwamba utufikishie salamu na utusaidie kusukuma tupate fedha za kumalizia shule hii na miradi mingine kadhaa ambayo tunataka ije Kata ya Kisiwani

"Kubwa ni ombi la ardhi, hii ardhi hapa ilipo alijitolea mzee wetu Manofu na kijana wake Said ,Tunawashukuru sana ,lakini eneo hili halitoshi kama ulivyofahamishwa zilizopo ni heka tatu lakini tumeomba watuidhinishie heka 10 nyingine ili tukamilishe mradi kwa viwango vilivyokusudiwa . nikuombe utusaidie kusukuma hili wananchi hawa Watoto wao wanapata shida na huu ni mwanga mzuri

"Pamoja na hayo tunaomba utufikishie salamu zetu kwa Rais Samia Suluhu Hassan haya yanayotokea yalikuwa ndoto kwao kwa miezi kadhaa iliyopita lakini chini ya uongozi wake yanakwenda kutokea ,Kama alivyosema diwani sisi tutakufa naye mwaka 2025 kwa mara nyingine Katibu Mkuu karibu kisiwani, karibu Muheza,"amesema.Mbunge Mwana FA.
Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV- Tanga

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amefanya ziara katika Wilaya ya Muheza mkoani Tanga ambapo pia amepata nafasi ya kukagua miradi ya maendeleo ukiwemo wa ujenzi wa Shule ya Sekondari inayojengwa Kata ya Kisiwani.

Akizungumza na Wananchi akiwa katika Kata ya Kisiwani wilayani Muheza mkoani Tanga , Chongolo amesema Serikali inayosimamiwa na Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa kwenye eneo la elimu na kwamba ujenzi wa Shule za Sekondari unaendelea maeneo mbalimbali nchini.

"Ujenzi wa Shule za Sekondari hauko hapa Kisiwani peke yake bali unafanyika nchi nzima kwenye kila Wilaya.Shule nyingi zinajengwa zaidi ya 200 nchi nzima, kwa kutolewa fedha zote na Serikali kwa ajili ya kusogeza elimu kwa wannanchi,hiyo ndio kazi ya Serikali na bahati mbaya watu hawazisemei na kuonesha kwamba hizi shule zinajengwa na kazi kubwa inafanyika

"Lakini sisi tunapita kujiridhisha na kiwango cha ubora, kuona kama fedha zimefika, matumizi yake,huduma kama inaenda kusogezwa kwa wananchi au inaenda kupendelea eneo fulani, hapa tumejiridhisha uamuzi wa kuijenga shule hii hapa ulilenga dhamira ya kusogeza elimu kwa Wananchi,hongereni sana ,mmeniambia hapa kuhusu changamoto ya ardhi na kwa mazingira kama haya tuweka kidato cha Tano na Sita wanafunzi wetu watakuwa na uhakika wa kusoma vizuri sana ,hiii hali ya hewa inaruhusu

"Mazingira ni mazuri,hii shule iko kwenye mazingira rafiki kwa nwanafunzi kujitafutia na kutumia muda mwingi kusoma, shule inafaa iongezewe msukumo wa kuongozewa eneo ili lipatikane eneo la kuja kujenga bwalo ,kujenga madarasa mengine ya kidato cha Tano na Sita lakini kujenga nyumba za kutosha za walimu,"amesema Chongolo.

Ameongeza kuwa hivyo atakwenda kusuma ajenda ya kupata fedha Sh.milioni 130 kwenye shule zote kwa lengo la kujenga nyumba za walimu na kwamba fedha hizo zinatosha kujenga nyumba nne kwa moja badala ya kujenga nyumba moja au mbili. Ni lazima watengeneze msukumo wa kutumia hizo edha vizuri ili zienga nyumba nyingi kuliko hata ramani walizopewa.

"Hakuna ramani itakayogambana na wingi wa nyumba,nyumba zikiwa zimewekwa tatu ninyi mkaweka nyumba nne hakuna atakayekuja kuleta hoja kwanini mlijenga nyingi,shida mkipunguza mkajenga chache.Niwapongeze wananchi ninyi ni watu bingwa sana mmeonesha kwa namna mnavyoenda maendeleo.

"Hapa mmechangia zaid ya Sh.milioni 27 fedha ambazo zimetokana na nguvu kazi yenu lakini na michango yenu wenyewe kabla ya uamuzi wa Rais na Serikali anayoiongoza kuleta fedha, hongereni sana, lakini nimezungumza kujengwa kidato cha Tano na Sita ,nimesema ijengwe hapa kwasababu tayari Serikali imefanya uamuzi wa kutoa elimu bila malipo kwa kidato cha Tano na Sita ili kupanua na kuongeza wigo wa vijana wetu kupata fursa ya elimu bila malipo kuanzia darasa la awali hadi kidato cha Sita,"amesema.

Ameongeza lengo lake ni nini, wengi wanasema elimu bure maana yake hamna anayelipia lakini hiyo elimu bila malipo kwa wananchi kwasababu malipo yanatolewa na Serikali.

"Narudia tena tunaita elimu bure tunakosea bali ni elimu bila malipo kwa maana ya mwanannchi halipi lakini Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa ile elimu badala ya mwananchi au kwa niaba ya mwananchi kwa maana kuna watu wanasema imetokea miujiza, shule zinajiendesha kwani hakuna walimu,walimu wanakuja bure shuleni?


"Nimepata maelezo ya mzee aliyeamua kutoa ardhi kwa ajili ya elimu sio jambo dogo ni jambo la heshima basi hata jina la shule mumpe yule mzee ili iwe kumbukumbu ya kizazi na kizazi kwamba pamoja na kwamba ametoa ardhi kwa hiyari yake lakini kukumbuka ya familia kwamba hapa palikuwa kwa nani ni jina waliyoipa shule , tujenge tabia ya kuthamini anachofanya mtu, tujenge tabia ya kuheshimu na kutoa mchango na sisi kumheshimu aliyefanya kitu fulani, napendekeza hii shule iitwe Manofu Sekondari kutambua mchango wa mzee wetu Manofu ambaye ametoa ardhi yake,".
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo na ujumbe wake wakikagua baadhi ya majengo ya mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kisiwani iliyopo kata ya Kisiwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza mbele ya Katibu MKuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo pamoja na Wananchi mbalimbali akimpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akiendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.Pichani kushoto ni Mbunge wa jimbo la Muheza Mh.Hamis Mwinjuma.
Mbunge wa jimbo la Muheza Mh.Hamis akizungumza mbele ya Katibu MKuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo pamoja na Wananchi mbalimbali akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akiendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ndani ya jimbo lake.PICHA NA MICHUZI JR-TANGA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Ndugu Omary Mgumba (kushoto) mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kisiwani iliyopo kata ya Kisiwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamis Mwinjuma pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Ndugu Omary Mgumba (kushoto) mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kisiwani iliyopo kata ya Kisiwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamis Mwinjuma mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kisiwani iliyopo kata ya Kisiwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo (katikati) akiwa na ujumbe wake pamoja na mkuu wa Mkoa Mhe.Omari Mgumba (kulia) wakielekea kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kisiwani iliyopo kata ya Kisiwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.PICHA NA MICHUZI JR-TANGA

Moja ya Jengo la shule ya Kisiwani likiwa mbioni kukamilika

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo na ujumbe wake wakikagua baadhi ya majengo ya mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kisiwani iliyopo kata ya Kisiwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...