KATIKA kulifikia soko la asali na mazao mengine ya nyuki ndani na nje ya nchi wadau wa bidhaa hizo wamewashauri mbinu za kisasa katika ufugaji na uvunaji ili kuweza kupata asali inayokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

Ushauri huo umetolewa leo Agost 4 Dar es Salaam katika semina ya mradi wa Intenational Trade Centrer iliyowakutanisha wadau wa asali na mazao mengine ya Nyuki lwa lengo la kuwafundisha mbinu bora za kutumia katika ufugaji ili kupata asali yenye ubora itakayopata soko ndani na nje ya nchi.

Imeelezwa kuwa asali inayozalishwa hapa nchi inashindwa kupata soko la uhakika nje ya nchi kutokana na viwango vyake.

Fatma Mwiniko Afisa Viwango kutoka Shirika la Udhibiti Viwango nchini (TBS) amesema shirika hilo limehudhuria kwenye semina hiyo ili kuwapa elimu ya wafugaji juu ya ubora na usalama ili kuendana soko la ndani na la nje ya nchini.

"Tunamatumaini Semina hii itawanufaisha wafanyabiashara , wafugaji na wasafirishaji wa asali kuvifikia viwango vya asali vya ndani na nje"

Kufutlia hali hiyo akatoa rai kwa wafugaji asali kuzingatia ubora kwenye ufugaji ili wapate tija ya zao hilo.

Seif Salum ofisa wa Ufugaji nyuki kutoka Taasisi ya Apps Support amesema amesema kuwa ili viwango vya asali viwe vinaridhisha ni lazima ubora uanzie kwa mfugaji.

"Masoko yetu yanahitaji sana viwango katika kufikia viwango vya mazao ya nyuki kwanza kifaa kinachitumika kama mzinga au eneo unalofugia linakemikali nyingi asali hiyo haitakuwa bora"

"wafugaji lazima wahakikishe kwamba wanatumia mbinu za ufugaji bora mfano mizinga bora kutofuga kwenye eneo linalotumika kwenye kilimo na mifugo au eneo lenye viwanda amabalo kemikakali nyingi zinatoka"

Amesema licha ya kuzingatia ubora kwenye ufugaji pia ni lazima wafugaji watumie vifaa vya kisasa, mavazi mazuri ya kinga, vifungashio na uachakataji sahihi.

Amesisitiza kuwa wananchi wengi hawana uelewa juu ya ubora wa asali ukizingatia wao ndio watumiaji huku akiweka bayana kuwa wanatakiwa wajue ili waelewe kiasi halisi cha maji yanayotakiwa kutumika kwenye Asali.

Philip Ofisa mfugaji mkuu wa nyuki kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS) amesema kuwa TFS ni sehemu ya mradi huo na kwamba semina hiyo inawafundisha wafugaji juu ya changamoto za kusafirisha mazo ya nyuki zinazopelekea kufujisha viwango vya asali.

Amesema kuwa katika matokeo mradi huo watakaonufaika ni pamoja na taasisi za mafunzo , na kwamba watakaofaidika moja kwa moja wafugaji, wafanyabiashara, taasisi za kibiashara.

"Moja tuliojifunza leo ni kusimamia ubora wa mazo ya nyuki ambayo ni changamoto inayosababisha kutofanya vizuri kwenye masoko ya nje"amesema Philip.

Amesema kuwa hatua za ubora zinaanza kwa mfugaji, wachakataji mwisho kwa wasafirishaji nje ambapo kwenye hatua hizo kunaweza kupoteza ubora na viwango endapo uchakataji hajawa nzuri.

Josephe Kadindula Mwenyekiti wa Jukwaa la wasafirishaji wa bidhaa za mazao ya nyuki amesema kuwa Semina hiyo imewasaidia kujua viwango vya asali vinavyokubalika kwenye soko la dunia.

Amesema kuwa hali ya uhitaji ya bidhaa hiyo inaridhisha "Hali ya uhitaji wa asali katika soko la nje ni kubwa kwa hiyo tunatakiwa kuwa na ubora ili kukidhi bidhaa zetu kukubalika nje"
Fatma Mwiniko Afisa Viwango kutoka Shirika la Udhibiti Viwango nchini (TBS)  akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 4,2022 jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza warsha ya siku tatu ya kujenga uwezo kwa wafugaji nyuki ili kuboresha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki na kupata asali yenye viwango vya ubora unatakiwa na soko la dunia Warsha hiyo imeandaliwa na Shirika la Kimataifa la biashara ICT.
Filipe Ndilahomba, Ofisa mfugaji mkuu wa nyuki kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania  TFS) akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 4,2022 jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza warsha ya siku tatu ya kujenga uwezo kwa wafugaji nyuki ili kuboresha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki na kupata asali yenye viwango vya ubora unatakiwa na soko la dunia Warsha hiyo imeandaliwa na Shirika la Kimataifa la biashara ICT.
Seif Salum ofisa wa Ufugaji nyuki kutoka Taasisi ya  Apps Support 
akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 4,2022 jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza warsha ya siku tatu ya kujenga uwezo kwa wafugaji nyuki ili kuboresha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki na kupata asali yenye viwango vya ubora unatakiwa na soko la dunia Warsha hiyo imeandaliwa na Shirika la Kimataifa la biashara ICT.
Joseph Kadendula Mwenyekiti wa Jukwaa la wasafirishaji wa bidhaa za mazao ya nyuki  akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 4,2022 jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza warsha ya siku tatu ya kujenga uwezo kwa wafugaji nyuki ili kuboresha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki na kupata asali yenye viwango vya ubora unatakiwa na soko la dunia Warsha hiyo imeandaliwa na Shirika la Kimataifa la biashara ICT.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...