Na Janeth Raphael
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt Pindi Chana amewaasa makamanda, maafisa na Askari wa uhifadhi (TFS) kushirikana na wadau mbalimbali katika kutatua kero za uhifadhi na kutatua migogoro baina ya wananchi na uhifadhi nchini.
Akizungumza leo Agosti 29,2022 jijini Dodoma katika Mafunzo ya makamishna, makamanda na askari wa uhifadhi wa misitu ya Kila mwanzo mwa mwaka wa fedha, ambapo amewataka Makamanda, Maafisa na Askari hao kusimamia sheria pamoja na kutowaruhusu wavamizi wasipewe nafasi kuingia katika hifadhi za Misitu kwa maendeleo ya Taifa na watu wake.
"Shirikianeni na kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya kuhakikisha wavamizi wote wanaondoka na kuacha hifadhi za misitu zikiwa salama, ndugu zangu jambo hili la uvamizi katika maeneo ya misitu tusiliruhusu na hili ni eneo ambalo tutawapima" Amesema Dkt Pindi
Aidha, Dkt Pindi amesema ili kuwa na misitu bora nikuilinda na kuihifadhi ili kuziwezesha sekta nyingine kukua huku akiwaomba askari hao kutumia silaha kwa utaratibu mzuri ili kulinda heshima ya jeshi la uhifadhi.
"Ndugu viongozi na makamanda nyinyi nyote mnao wajibu wa kulinda na kuendeleza Rasilimali za misitu na nyuki,hili ni jukumu la msingi ambalo mbinu za kijeshi zinatakiwa kuwezesha kufikia lengo hili yani kuwa na misitu bora katika kuziwezesha sekta zingine kukua" Amesema Dkt pindi chana.
Kwa upande wake Prof. Vedastus Silayo Kamishna wa uhifadhi wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) ameitaja changamoto ya kuongezeka kwa tishio ya kiusalama na ongezeko la wananchi kujichukulia sheria mkonono jambo ambalo linalopelekea kujeruhiwa na kuuawa kwa baadhi ya askari na maafisa wakati wakitekeleza majukumu yao.
"Ni changamoto kubwa sana na hizi siku za karibuni matukio haya yamekuwa yakiongezeka sana lakini kama jeshi la uhifadhi tumejipanga katika kukomesha vitendo hivi, lakini pia kuongezeka kwa vyombo vya usafiri hususani pikipiki katika maeneo ya uhifadhi nayo pia ni changamoto kubwa sana na changamoto hii tunaendelea kuifanyia kazi kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali zinazosimamia vyombo hivi."Amesema Prof. Silayo.
Dhamira ya wakala wa Huduma za misitu Tanzania(TFS) ni kuwa na usimamizi endelevu wa rasilimali za kitaifa za misitu na nyuki ili kuchangia mahitaji ya kijamii, kiuchumi, kiikolojia na kiutamaduni kwa kizazi cha sasa na kijacho”.

Baadhi ya Makamishina, makamanda na askari wa uhifadhi wa misitu wakiwa katika mafunzo hayo leo yaliyofanyika jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...