Na. Damian Kunambi, Njombe.

Kutokana na baadhi ya wananchi wilayani Ludewa mkoani Njombe kuishi katika maeneo ya pembezoni na kupelekea watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu katika kutatua changamoto hiyo serikali ipo katika mchakato wa kujenga shule tatu katika kata ya Mlangali, Mavanga pamoja na Ludewa mjini ambayo itajengwa katika eneo la Mdonga.

Akuzungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mavanga mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema kuwa maeneo mengi ya jimboni kwake huduma za shule zimekuwa chache hivyo baadhi ya wanafunzi hutembea kilometa nyingi kitu ambacho huwafanya washindwe kusoma vizuri na kusababisha utoro.

Amesema kwa sasa amefanikiwa kupatiwa shule hizo tatu lakini ataendelea kuiomba serikali impe shule nyingine tena ili kuhakikisha watoto wote wa jimboni kwake wanapata elimu pasipo kuteseka.

Sanjari na hilo pia mbunge huyo amechangia kiasi cha sh. Ml. 1.4 kwaajili ya utengenezaji wa vitanda katika shule ya sekondari Mavanga, mipira mitatu kwa timu za vijana pamoja na blanket kwa mzee mmoja.

"Serikali inafanya juhudi ya kuhakikisha kiwango cha elimu kinapanda kote nchini, nasi pia tunapaswa kuungana na serikali katika maendeleo hayo hivyo napenda kuwaasa wanafunzi wasome kwa bidii kwakuwa serikali imewekeza fedha nyingi kwao",. Amesema Kamonga.

Aidha kwa upande wake kaimu Afisa elimu Msingi amekiri kuwepo kwa mchakato huo na kuongeza kuwa kuna wanafunzi wengi ambao hukaa mbali na shule (shule mama) hivyo ujenzi wa shule hizo zitasaidia kuinua kukuza kiwango cha elimu.

 

 Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga (aliyeshika ngoma) akiburudika pamoja na wananchi wakati wa mapokezi yake katika kata ya Mavanga.

Mke wa mbunge wa jimbo  la Ludewa Joseph Kamonga(kushoto) akimkabidhi fedha mpokea michango ya shele ya Sekondari Mavanga.
Viongozi wa timu mbalimbali za kijiji cha Mavanga ili kuboresha michezo.
Mbunge wa jimbo la Ludewa ( kulia) akimsikiliza mmoja wa wazee wa kijiji cha Mavanga alipokuwa akiongea baada ya kukabidhi zawadi ya blanket na mbunge huyo
Mbunge wa jimbo la Ludewa (Kushoto)akipiga zeze mara baada ya kuwasili katika kata ya Mavanga.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...