Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wameingia mkataba wa makubaliano wa zaidi ya Shilingi Bilioni 26 (Tsh. 26,168,005,000/-) na Kampuni ya Michezo ya Kubashiri (M-Bet) ikiwa ni mkataba wa miaka mitano baina ya pande zote mbili kati ya Klabu hiyo na Kampuni hiyo.

Katika mkataba huo wa makubaliano kila mwaka timu hiyo itapokea kiasi cha fedha ambacho kipo kwenye makubaliano ya mkataba huo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Barbara Gonzalez amethibitisha kuwa mkataba huo ni kwa timu ya wakubwa pekee, huku akisema timu nyingine za Vijana na Wanawake zinatafutiwa Mdhamini wake tofauti na awali, Mdhamini Mkuu alikuwa akidhamini timu zote.

“Hii ni mara ya kwanza Mdhamini mkubwa anakuwa na ‘senior team’ pekee, huko nyuma mdhamini mkuu alikuwa kwa timu zote, lakini sasa timu zingine tunaweza kuzitafutia mdhamini wake”, amesema Barbara 

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu hiyo, Salim Abdallah (Try Again) amesema baada ya makubaliano hayo na Kampuni hiyo, kwa haraka walipata kiasi cha fedha Shilingi Milioni 400 kwa ajili ya kufanya usajili kuelekea msimu ujao wa mashindano.
 
Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi amesema wameingia mkataba wa makubaliano na Simba SC ili kuleta maendeleo ya mpira wa miguu nchini Tanzania, hata hivyo wanajivunia kuwa na ushirikiano na timu kubwa hapa nchini, Simba SC kutokana na wao kuwa na uwakilishi katika mataifa kadhaa barani Afrika.

Katika makubaliano hayo, mwaka wa kwanza Simba SC itapata kiasi cha fedha Shilingi Bilioni 4.670, mwaka wa pili watapata Shilingi Bilioni 4.925, mwaka wa tatu Shilingi Bilioni 5.205, mwaka wa nne Bilioni 5.514 na mwaka wa tano watapokea kiasi cha Shilingi Bilioni 5.853.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...