* Wapata fursa ya kutangaza bidhaa, kupata masoko
WAFANYABIASHARA kutoka Tabata na
maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam wamekutana kupitia maonesho ya
biashara ya ‘Tabata Pop Up’ na kupata fursa ya kutangaza bidhaa pamoja
na kubadilishana uzoefu ili kujijenga vizuri kibiashara.
Akizungumza
katika maonesho hayo mjasiriamali Debora Mavura ambaye ni muandaaji wa
Tabata Pop Up lakini pia mzalishaji na muuuzaji bidhaa za Dekit
Slippers (Malapa ya kutembelea ndani) amesema maonesho hayo ya biashara
yamefanyika kwa lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara na kupata fursa
ya kutangaza bidhaa zao pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu ili
kujijenga zaidi kibiashara na kupata fursa za masoko.
Bi. Debora
amesema kukutana kwa wafanyabiashara hao kutasaidia kutangaza na
kuonesha bidhaa zao katika soko la Tabata na maeneo mengine pamoja na
kubadilishana mawazo ya kukuza zaidi biashara zao.
‘’Soko la
Tabata ni kubwa, kuna vitu na watu wengi. Kwa kipindi kifupi sana jina
la tabata limekua Kwa Kasi kubwa, hii ni Moja ya sababu iliyomfanya bi.
Debora kuona fursa chanya na kuitumia Ili kuweza kuonesha jamii ya
tabata na nje ya tabata vitu vizuri na vya maendeleo vinavyoweza
patikana tabata, ikiwemo hivi tunavyoonesha leo. Tabata Kuna fursa
mbalimbali na kwa kupitia vijana kutoka hapa Tabata na maeneo mengine
tutaendelea kuhamasishana katika kushiriki katika maonesho haya ya
kutangaza bidhaa ili kuweza kujijenga zaidi katika biashara na masoko
kwa ujumla.’’Amesema.
Bi. Deborah amesema amekuwa akishiriki
maonesho mbalimbali ya ujasiriamali na kuzichukua changamoto kama fursa
ambazo kwa kukutana na wajasiriamali hao watapeana elimu na mwelekeo wa
kuboresha biashara zao.
Aidha amesema kuwa wataendelea kukutana
kupitia maonesho ya namna hiyo ili kupata nafasi ya kujitangaza pamoja
na kujikuza kibiashara na kuweza kuwainua vijana wengine.
Maonesho
hayo yamehusisha washiriki kumi waliopata fursa ya kutangaza bidhaa
mbalimbali ikiwemo mavazi, bidhaa za ngozi, vipodozi pamoja na vinywaji.
Baadhi
ya washiriki wa maonesho hayo wameshukuru kwa ushirikishwaji katika
maonesho hayo ya Tabata Pop Up na kuomba uendelevu wa maonesho ya namna
hiyo ambayo husaidia zaidi katika kutangaza bidhaa zao na kupata masoko.
Mfanyabiashara wa bidhaa za urembo Glory Kimaro (kulia,) akimuhudumia mteja aliyekuja kupata huduma katika maonesho hayo ya kutangaza bidhaa yaliyowakutanisha wafanyabiashara kutoka Tabata na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam.
Muonekano wa baadhi ya bidhaa.
Mfanyabiashara wa nguo na bidhaa za kike Nice Magesa (kushoto,) akibadilisha mawazo na Doreen Frowin ambaye ni mfanyabishara wa nguo za kike katika maonesho ya kutangaza bidhaa yaliyowakutanisha na kufanyika katika viwanja vya Nyantare Tabata jijini Dar es Salaam.
Muandaaji wa maonesho hayo Debora Mavura (kushoto,) akiwa na mmoja ya washiriki wa maonesho hayo ya kutangaza bidhaa maarufu kama Tabata Pop Up yaliyofanyika katika viwanja vya Nyatare jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa bidhaa za ngozi zinazozalishwa na kusambazwa na kampuni ya AMIMETA VENTURES LTD ya jijini Dar es Salaam.
Mfanyabishara wa bidhaa za ngozi kutoka kampuni ya AMIMETA VENTURES LTD Adam Niyonzima akiwa katika maonesho hayo ya kutangaza bidhaa yaliyowakutanisha wafanyabiashara kutoka Tabata na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam.
Mfanyabiashara wa vifaa vya umeme Prince Enock akipanga bidhaa wakati wa maonesho ya kutangaza bidhaa 'Tabata Pop Up' yaliyowakutanisha wafanyabiashara kutoka Tabata na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam.
Maonesho ya bidhaa yakiendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...