Na Mwandishi Wetu, Arusha

TANZANIA ipo katika nafasi nzuri ya kuwa mzalishaji mkubwa wa mbogamboga na matunda barani Afrika endapo itaitumia vizuri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti na Uendelezaji wa Kilimo cha Mboga Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika kinachojulikana kama ‘World Vegetable’ Center.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kujifunza shughuli mbalimbali za Taasisi hicho cha kimataifa chenye Makao Makuu Jijini Arusha , Mkurugenzi wa Taasisi hiyo , Dkt. Gabriel Rugalema alisema taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi ya kukusanya, kuchakata na kutunza mbegu za mazao ya mbogamboga, viungo na vikolezo pamoja na mazao ya matunda.

“ Mazao mengi hayana utafiti mkubwa katika Bara la Afrika na ndipo tuliona tuanze kufanya utafiti hapa Tanzania, ili tuwe na mbegu zetu za asili sambamba na kufanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo ili kuzalisha mbegu bora za kisasa kwa ajili ya kilimo cha mazao hasa ya mbogamboga,” alisema Dkt. Rugalema.

Alisema Kazi waliyopewa na Serikali ni kufanya utafiti wa mbegu mama, utafiti ukishakamilika mbegu hizo zinapelekwa kwenye vituo vya utafiti vya serikali kama Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) , wakala wa Taifa wa uzalishaji na uendelezaji wa mbegu za kilimo (ASA) pamoja na Taasisi binafsi kwa ajili ya kuziendeleza na kusajiliwa na Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu (TOSCI) kwa ajili ya kuzipeleka sokoni.

‘’ Nipende kuipongeza serikali kwani imekuwa ikiendelea kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuwa na uhakika wa usalama wa chakula, kukuza kipato cha mwananchi sambamba na kuzalisha ajira kwa wananchi hususani wanawake na vijana,’’ alisema Dkt. Rugalema.

Naye Mtafiti wa Mbegu, Bw. Jeremiah Sigalla alisema kituo hicho kina uwezo mkubwa wa kutafiti mbegu mbalimbali na kutoa mchango stahiki katika sekta ya kilimo ndani na nje ya Tanzania.

alieleza majukumu ya kituo hicho ni pamoja na kuhakikisha tafiti za mazao ya mboga zinafanyika ili kuifanya nchi na mataifa jirani kupata uhakika wa mbegu mbalimbali za mboga sambamba na kutunza kwenye benki ya mbegu ikiwa na lengo la kutopoteza utofauti wa mbegu kwa ajiri ya kizazi cha sasa na baadaye.

“Mpaka sasa benki yetu ina zaidi ya mbegu tofauti tofauti elfu nne, ikiwemo mbegu ya mchicha ikiwa na aina mia nne na bamia ikiwa na aina elfu moja mia sita,” alisema Bw. Sigalla Na kuongeza kuwa idadi hiyo inabadilika kila mwaka kutokana na muendelezo wa ukusanyaji mbegu kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Kwa upande wake, Mratibu wa mafunzo na ugani Bw. Hassan Mndiga alisema mbali ya kutafiti, kuzalisha na kutunza mbegu, Kituo kimekuwa kikitoa mafunzo kwa watu toka mataifa mengi barani Afrika na nje ya bara la Afrika.

Mbali ya kutafiti,kuzalisha na kutunza mbegu, Taasisi hiyo ina shamba darasa kwaajili ya kuwafundishia vijana waliohitimu vyuo vikuu mbalimbali mbinu za kiushindaji wapojiajiri au kuajiriwa kwenye makampuni.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti na Uendelezaji wa Kilimo cha Mbogamboga Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (World Vegetable center), Dkt. Gabriel Rugalema (kulia) akitazama mbegu za mboga mboga zimazotunzwa kwenye benki ya mbegu ya kituo hicho ambacho mpaka sasa kimehifadhi aina tofauti 4,000 za mbegu za mbogamboga na matunda (kushoto) ni Mtafiti wa Mbegu, Bw. Jeremiah Sigalla.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti na Uendelezaji wa Kilimo cha Mbogamboga Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (World Vegetable center), Dkt. Gabriel Rugalema akielezea namna wanavyootesha mbegu kwenye moja ya kitalu nyumba kilichopo makao makuu ya kituo hicho eneo la Tengeru Jijini Arusha jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...