Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Baadhi
ya maeneo Halmashauri ya Mji Kibaha, Mkoani Pwani yanakabiliwa na kero
ya Ukosefu wa maji ya uhakika kwa takriban mwezi mmoja Sasa hali
inayosababisha kero kwa wananchi.
Kutokana
na kero hiyo, Baraza la madiwani Kibaha Mjini , limeitaka Mamlaka ya
maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA )kuweka mipango ya muda
mrefu kutatua kero hiyo inayojirudia Mara kwa Mara.
Akiuliza
swali la papo kwa papo na kulielekeza Taasisi ya maji DAWASA katika
Baraza la madiwani Kibaha Mjini ,diwani wa kata ya Mbwate ,Fokas Bundala
alieleza ,wanapata tabu ya upatikanaji wa maji ya uhakika ,kwa muda
mrefu sasa bila kuwa na majibu ya kina.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha ambae pia ni Diwani wa Sofu Mussa
Ndomba alieleza ,inasikitisha chanzo Cha Ruvu na Mlandizi Vipo Kibaha
,Pwani Lakini maji hayapatikani kwa uhakika huku Dar es Salaam wakipata
maji.
"Tunasubiria maji
usiku, unakuta mtu anaangalia kipindi cha TV hata kama hapendi kuangalia
ili asubirie maji, chanzo kipo kwetu ,Lakini tunapata maji kwa shida
kama tupo pembezoni mwa mji kumbe Mjini,na tatizo hili limekuwa la
kujirudia"alifafanua Ndomba.
Nae
Diwani wa Visiga, Kambi Legeza alitaja kero nyingine, ni wateja
waliolipia vifaa na kuunganishiwa maji kushindwa kufikishiwa huduma
kipindi kirefu takriban mwaka mzima sasa .
"Wateja wengi wamelipia lakini tatizo vifaa,je ofisi yenu DAWASA inakwama wapi,alihoji Kambi.
Hata
hivyo Kambi ,alitaka pia DAWASA kuangalia namna ya kupunguza mzigo kwa
miradi ya RUWASA ambapo wananchi wanalipia mara tatu huku DAWASA
ikitakiwa kuipokea baada ya ujenzi.
Diwani
viti maalum Kibaha Mjini,Selina Wilson aliitaka DAWASA kusimamia tatizo
linalodaiwa na baadhi ya wananchi kulalamikia kubambikiwa bill suala
ambalo linaondoa uaminifu .
Vilevile,
kushughulikia mafundi vishoka na mafundi ambao wameshawaondoa kazini
wajulikane na wasiendelee kupita kwa wateja na kutumia mwamvuli Kuwa
bado watumishi.
Alisema ,Shirika la Umeme TANESCO lipo kwenye matengenezo ya muda mfupi na watakapokamilisha tatizo linaisha.
Akielezea
suala la wateja ambao wameshalipia vifaa kutounganishiwa huduma ya maji
kwa wakati , Yohana alieleza ,maombi ya wateja ni mengi ,muitiko mkubwa
tofauti na lengo lao hivyo wamejipanga kuanza na wateja ambao wamelipia
tangu mwezi Mei mwaka huu na baadae wataendelea na wateja wapya.
Kuhusu
, tatizo la maji shule ya Sekondari Viziwaziwa , Pichandege na Msangani
alisema kwamba, wanafanya marekebisho kwenye miradi maeneo yenye
uhitaji wa kurekebishwa na kutengeneza na kuboresha miundombinu awamu
kwa awamu kulingana na miradi lengwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...