Katika jitihada za kutafuta fursa mbalimbali za ajira kwenye sekta ya afya, ujumbe wa Tanzania uliopo ziarani nchini Qatar umekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Hamad Medical Corporation (HMC) Jijini Doha, Qatar.

Ujumbe huo wa serikali uliongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu kwa kushirikiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab.

Viongozi hao wamejadiliana namna ya kuanza kutoa nafasi za ajira kwa watanzania. Watalaam wa sekta ya Afya nchini Tanzania walikuwa hawajaanza kuingia kwenye soko la ajira la Qatar na hivyo endapo Tanzania itafunguliwa nafasi hizo itaweza kupeleka watalaamu wake kufanya kazi nchini humo.

Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi, Idara ya Rasilimali Watu wa 'Hamad Medical Center', Bi. Sabeeha Amin Qasemi amesema kuwa hospitali hiyo imefurahishwa na hatua ambazo Tanzania inazichukua katika kuboresha sekta ya afya na kuahidi kuwa watatoa nafasi za ajira kwa wataalamu wa afya ambao hatimaye watapelekwa kwenye hospitali mbalimbali nchini Qatar.

Naye, Prof. Katundu ameuhakikishia uongozi wa Shirika hilo kuwa Tanzania ina wataalamu wa afya wenye uwezo na uzoefu wa kutosha na endapo watapata fursa za ajira nchini humo watafanya kazi kwa bidii na weledi kwa kuzingatia sheria na taratibu za Qatar kwa kuwa watahiniwa hao hupatiwa mafunzo wakati na baada ya usaili wa ajira.

Kwa upande wake, Balozi Fatma Rajab amesema kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Qatar ili kuiwezesha Serikali hiyo kupata wafanyakazi bora zaidi katika sekta mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi, Idara ya Rasilimali Watu wa 'Hamad Medical Corporation', Bi. Sabeeha Amin Qasemi akizungumza na ujumbe wa Serikali ya Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu kwa kushirikiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab walipokutana kwa mazungumzo Jijini Doha, Qatar




Mmoja wa Mawakala wa ajira binafsi kutoka Tanzania akichangia jambo wakati wa mazungumzo ya vuiongozi hao yaliyofanyika Jijini Doha, Qatar


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akielezea mkakati wa Serikali kwa uongozi wa 'Hamad Medical Corporation' Jijini Doha, Qatar. Wa kwanza kulia mwa Prof. Katundu ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab



Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akielezea mkakati wa Serikali kwa uongozi wa 'Hamad Medical Corporation' Jijini Doha, Qatar

Mazungumzo baina ya Ujumbe wa Tanzania na Uongozi wa Hamad Medical Center yakiendelea Jijini Doha, Qatar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...