Tanzania imefanikiwa kuongezewa idadi ya vijana wanaoshiriki mafunzo ya kilimo kwa vitendo nchini Israel kutoka idadi ya Vijana 80 mpaka 250.

Hayo yamesemwa jana Jerusalem,Israel na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Israel-MASHAV Bi. Eynat Shlein katika mazungumzo yake na Naibu Waziri wa Kilimo Mh.Anthony Mavunde wakati wa mahafali ya Vijana zaidi ya 1300 kutoka mataifa 12 waliopata mafunzo ya kilimo na ufugaji kwa vitendo.

“Sisi na Tanzania tumekuwa na uhusiano mzuri kwa muda mrefu,na uhusiano huu umeongezeka maradufu chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan,hali ambayo imepelekea kuona umuhimu wa kuiongezea Tanzania nafasi zaidi va vijana kuja kushiri mafunzo ya kilimo na ufugaji kwa vitendo kutoka idadi ya vijana 80 kwa mwaka 2021/2022 mpaka 250 kwa mwaka huu, ambao tunaamini watasaidia sana kuleta mchango mkubwa katika ukuaji wa sekta ya kilimo Tanzania”Alisema Bi Eynat

Naibu Waziri Mavunde ameishukuru nchi ya Israel kwa mchango mkubwa inautoa katika kusaidia kukuza sekta ya kilimo nchini Tanzania kupitia ushiriki wa serikali na makampuni binafsi katika kusambaza elimu juu ya teknolojia bora na kanuni bora za kilimo chenye kuleta tija kwa wakulima wa nchini Tanzania.

Aidha Naibu Waziri Mavunde amewataka vijana hao kutoka Tanzania waliopata ujuzi katika masuala mbalimbali kuitumia elimu hiyo kukuza sekta ya kilimo nchini na kwamba serikali itahakikisha ujuzi walioupata haupotei bure na hivyo kuwashirikisha katika utekelezaji wa programu mbalimbali za serikali ikiwemo programu ya Vijana ya *Jenga kesho bora kupitia Kilimo *-(BBT)ambayo serikali imeanza utekelezaji wake katika mikoa ya Dodoma na Mbeya.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...