Na Mwandishi wetu, Mirerani
WACHEZAJI
wa kituo cha vijana cha Tanzanite Sports Academy cha Mirerani wilayani
Simanjiro ambacho kimekwenda jijini Dodoma kushiriki michuano ya vijana
ya Kashasha Youth tournament ambayo yameanza leo Alhamisi huku
yakipangwa kufikia tamati Jumapili hii, wamejinasibu kuwa watarejea na
ushindi.
Mkurugenzi wa
Tanzanite Sports Academy, Charles Mnyalu amesema mashindano hayo
yameandaliwa na Fountain Gate Academy ya jijini Dodoma ambapo yanatimua
vumbi kwenye uwanja wao wa Fountain Gate Arena.
Ameongeza
kuwa wamejindaa vyema kufanya kweli na kutwaa ubingwa kwani kutokana
na namna vijana hao walivyo hawaoni timu ya kuweza kuwazuia licha ya
kwamba lengo ni kuibua vipaji.
Amesema
mashindano hayo ni mazuri kwani ni daraja la kuvusha wachezaji wadogo
kisoka kupata fursa ya kuonyesha vipaji na kuweza kuonekana kwa mawakala
na vilabu mbalimbali ambayo inapelekea na wao kutimiza ndoto zao.
Mnyalu
ameweka wazi kuwa wameamua msimu huu timu zao mbili za vijana walio
chini ya umri wa miaka 13 na 20 kushiriki katika michuano hiyo ili
kuweza kuonyesha vipaji vyao lakini pia kuwakutanisha na wachezaji wengi
kutoka vituo tofauti kwani sera yao ni kutoa nafasi kwa vijana
kuonyesha vipaji vyao kwa ajili ya faida ya baadaye kwa Manyara.
“Kwa
muda mfupi ambayo kituo chetu imeanzishwa mafanikio makubwa yameonekana
kupitia katika mashindano kama haya ya vijana kwani tumeweza kumtoa
mlinda lango wa U-17 ambaye hivi sasa yuko nchini Uturuki kwa majaribio
kwenye moja ya timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza,” amesema Mnyalu.
Kwa
upande wake Mengi Laizer ambaye ni mtoto wa Bilionea wa madini ya
Tanzanite Saniniu Laizer amesema wapo katika mipango ya kurudisha morali
ya soka mkoani Manyara ambayo kwa sasa imepotea.
Mengi
akimwakilisha bilionea huyo katika halfa ya kuwaanga wachezaji wa kituo
cha vijana cha Tanzanite Soccer Academy cha Mirerani wilayani Simanjiro
ambacho kimekwenda jijini Dodoma kushiriki michuano ya vijana ya
Kashasha Youth tournament.
Mengi
amesema mikakati waliyonayo kwa sasa ni kuwaunga mkono wadau wote ambao
wameonyesha nia ya kufufua tena soka la Simanjiro ambayo lipo chini.
Ameongeza
kuwa kama wadau mchango wao ni kuhakikisha wanawashika vijana mikono
ili watimize ndoto zao huku akiunga mkono safari kwa kutoa Sh500,000 na
kuwataka kurudi na ushindi ambapo pia amewahidi kuendelea kuwawezesha
kupitia vifaa vya michezo.
Diwani
wa kata ya Naisinyai, Taiko Kurian Laizer amesema kama serikali kwa
kushirikiana na wadau hasa ambao wamegeukia soka la vijana anaamini
morali na hamasa ambayo imeshuka kwa sasa itarejea na kuwa kama zamani
ambapo walikuwa ni wilaya tishio kisoka Manyara.
"Hata
kwenye vikao vyetu vya baraza la madiwani nitaipeleka hii lakini pia
mimi mwenyewe nitajitahidi kushirikiana na wadau wa michezo ili wilaya
yetu irejeshe tena makali yake" amesema Taiko.
Katibu
mwenezi wa CCM Kata ya Naisinyai Simon Kinyasi amewaasa wachezaji hao
kutanguliza nidhamu kwani hakuna mafanikio yoyote bila kuwa na nidhamu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...