Taarifa ya familia imeeleza kuwa Marehenu Balozi Lweno amefariki leo alfajiri Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam alikokuwa anapatiwa matibabu na mazishi yatafanyika leo saa kumi Alaasiri.
Balozi Shani Lweno alisoma Shule ya Tabora Boys miaka ya 1960 na baadaye kuhitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1971 na mwaka huo huo aliajiriwa na Wizara ya Mambo ya Nje kama Afisa Ubalozi Conakry - Guinea. Baada ya hapo alifanya kazi katika Balozi za Tanzania Cairo - Misri, Khartoum - Sudan, Stockholm - Sweden, New York - Marekani na Addis Ababa - Ethiopia kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje. Mnamo mwaka 1993 aliteuliwa kuwa Balozi wetu Lusaka, Zambia mpaka alipostaafu mwaka 2003.
Baada ya kustaafu Alijiunga na timu ya Kitengo cha Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika iliyokuwa inasimamia Suala la Uhuru wa Sahara Magharibi. Baada ya mkataba wake kumalizika alirejea nyumbani. Balozi Lweno ameacha mke na watoto.
Mungu amlaze mahali pema peponi, Amin



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...