Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV - Moshi

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ametoa mwito kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini hususani mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kuhakikisha wanalinda Sekta ya utalii na kuthamini watalii wanaofika kwenye maeneo hayo.

Chongolo ameyasema hayo leo Agosti 3,2022 wakati akizungumza na Wanachama wa CCM, Moshi Mjini katika ziara yake mjini hapa, Chongolo amesema Utalii ukiyumba na Uchumi wa nchi unayumba hivyo amehimiza wananchi mbalimbali wanaohusika kwenye shughuli hizo za utalii kuhakikisha wanakuwa wakarimu kwa wageni.

“Rais wetu, Mama Samia katangaza utalii wetu ulimwenguni, na matokeo yake tumeyaona kwa idadi kubwa ya Watalii kufika nchini, hata Hoteli zetu zina uhakika wa kupata idadi kubwa ya Wageni wanaotoka sehemu mbalimbali duniani,” amesema Chongolo.

“Tuendelee kushiriki kwenye shughuli za utalii, kufanya kazi na Watalii bila kuwakera, kuwadokolea, bila kuwawekea vikwazo vya aina yoyote ili tuendelee kuwavutia waendelee kuja nchini pamoja na kuhamasisha wengine”, ameeleza.

Aidha,Chongolo amesisitiza kuwahudumia Watalii hao kwa busara na heshima kwa upendo na ukarimu kwa desturi ya Watanzania, amesema Serikali inaendelea kufanya kazi kubwa kuutangaza utalii ili kuongeza pato la taifa nchini na kupata Soko la kudumu kwa bidhaa zinazotengenezwa na vijana mbalimbali.

Pia, amehimiza vijana kutobweteka na kuchangamkia fursa kwa kujihusisha zaidi katika shughuli hizo za utalii kwa kufanya biashara ili kunufaika kwa njia kupata fedha kupitia Sekta ya Utalii.

Chongolo yupo mkoani Kilimanjaro katika mwendelezo wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 ya Chama cha Mapinduzi (CCM,) kuhamasisha uhai wa Chama pamoja na kuhamasisha ushiriki wa wananchi wa Kilimanjaro katika zoezi la Sensa itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu.


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo akizungumza na Wanachama wa CCM, Moshi Mjini katika mkutano wa ndani leo Agosti 3,2022 akieleza mambo mbalimbali ikiwemo kutoa mwito kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini hususani mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kuhakikisha wanalinda Sekta ya utalii na kuthamini watalii wanaofika kwenye maeneo hayo.




Wanachama wa CCM, Moshi Mjini wakiwa katika mkutano wa ndani leo Agosti 3,2022 wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo alipokuwa akizungumza nao mambo mbalimbali kuhusu chama sambamba na uchaguzi unaoendelea ndani ya chama hicho.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...