Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imefanya kikao cha Baraza la wafanyakazi leo ili kujadili mafanikio, mafanikio, changamoto na njia za kuweza kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa bajeti mwaka uliopita ya 2021/2022.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu Ununuzi na Ugavi Godfred Mbanyi amesema baraza ni chombo kinachoundwa na sheria ya Mahusiano kazini kwa ajili na kuweka mazingira mazuri mahali pakazi ambapo chombo hiki kinawiwa kwa mkataba baina na Menejimenti pamoja na chama cha wafanyakazi sehemu ya kazi.

Pia amasema baraza la leo limefanyika ili kutathmini utendaji kazi wa bajeti ya mwaka uliopita ya 2021/2022, kisheria na kiutaratibu bajeti yoyote kabla haijahidhinishwa lazima ipitishwe na Balaza la Wafanyakazi sehemu ya kazi.

Mbanyi amesema Bajeti ya mwaka 2021/2022 ilikamilika toka Juni 30 hivyo ni wajibu wa menejimsenti kuja kueleza balaza nini mafanikio, changamoto na  njia za kuweza kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa bajeti iliyokamilika muda wake.

“Umuhimu wa Mabaraza ya kazi kwanza yanaleta ushirikishwaji wa wafanyakazi sehemu ya kazi hivyo wafanyakazi wanakuwa ni sehemu ya maamuzi katika taasisi, kwaiyo taasisi sio kwamba inakuwa inaongozwa na Menejimenti lakini inakuwa na chombo ambacho kinawakilisha wafanyakazi wote katika taasisi mbalimbali.” Alisema Mbanyi

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi  akizungumza wakati wa kufungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB likilokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo lililofanyika leo Bagamoyo.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma wa PSPTB Amos Kazinza akitolea ufafanuzi kuhusu baadhi ya hoja zilizokuwa zinatolewa na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa PSPTB wakati wa kikao kilichofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani leo.
Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) , Amani Ngonyani akijibu hoja za wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa PSPTB ili kuboresha Utendaji kazi wa Bodi hiyo kwenye kikao cha Baraza hilo kilichofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.
Katibu mkuu wa TUGHE  Taifa, Hery Mkunda akitoa salamu  za uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania ( TUGHE ) wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB likilokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo lililofanyika leo Bagamoyo.
Mwenyekiti wa TUGHE PSPTB, Shilla Mwandu( wa kwanza kushoto) akizungumza kuhusu namna wafanyakazi wanabidi kujitadhmini pale wanapokuwa wanafanya kazi za Serikali wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB lililofanyika Bagamoyo mkoani Pwani.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa PSPTB wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa kwenye kikao kazi kilichokuwa na  lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo lililofanyika leo Bagamoyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi  akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bodi hiyo pamoja na wageni waalikwa wakati wa wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB likilokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo lililofanyika leo Bagamoyo mkoani Bagamoyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...