TANZANIA imejumuishwa kwenye orodha ya nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) zitakazonufaika na utekelezwaji wa Programu mpya ya Fit for Market Plus inayolenga kuwajengea uwezo wajasiliamali na wale wote wanaojihusisha na mnyororo mzima wa uongezaji thamani katika mazao ya kilimo, hususan mbogamboga na matunda ili waweze kuzalisha mazao na bidhaa za kilimo zinazokidhi viwango na mahitaji ya soko, hususan la Umoja wa Ulaya.

Programu hiyo inayotekelezwa na taasisi ya COLEACP kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya inazingatia Mkakati wa Umoja huo ujulikanao kama Farm to Fork Strategy unaolenga kudhibiti ubora wa bidhaa za mazao ya kilimo zinazoingia kwenye soko kuanzia shambani mpaka zinapomfikia mlaji wa mwisho.

Wizara inatoa wito kwa wadau wote wanaojihusisha na mnyororo wa uongezaji thamani katika mazao ya kilimo cha mbogamboga na matunda kuchangamkia fursa kwa kujitokeza kwa wingi kuwasilisha maombi yao ya kunufaika na utekelezwaji wa programu hii.

Wadau hao ni pamoja na kampuni na vikundi vinavyojihusisha na uzalishaji na uuzaji wa mazao ya mbogamboga na matunda; taasisi zinazojihusisha na utoaji mafunzo na ushauri wa kitaalamu kuhusu kilimo cha mbogamboga na matunda; mamlaka zenye dhamana ya usimamizi wa afya ya mimea; na taasisi za utafiti katika kilimo cha mbogamboga na matunda.

Kwa maelezo zaidi kuhusu namna ya kunufaika na utekelezwaji wa programu hii, wadau wanashauriwa kutembelea tovuti ya COLEACP: https://www.coleacp.org/current-programmes/fit-for-market-plus/. Wanaweza pia kuwasiliana moja kwa moja na COLEACP kupitia barua pepe support@coleacp.org.

Kupatikana kwa fursa hiyo ni jitihada za Ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji katika mikakati yake ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ambao unawahimiza pia wadau kutembelea tovuti: www.be.tzembassy.go.tz ili kupata taarifa zaidi kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye eneo la uwakilishi la ubalozi huo.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...