Na Janeth Raphael
WAKULIMA na wafanyabiashara wa Mbolea Kanda ya kati wametakiwa kuacha tabia ya kutumia Mbolea kiholela na badala yake waende kujifunza na kupata ushauri wa aina ya mbolea na matumizi yake ili wazalishe kwa Tija.

Hayo yamesema jijini Dodoma na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Kanda ya Kati Joshua Ng'ondya wakati akizungumza na Michuzi Blog kwenye banda la Mamlaka hiyo katika maonesho ya 28, Kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya nanenane eneo la Nzuguni ambapo Amesema kuwa ili wakulima waweze kuzalisha kwa tija wanatakiwa wajue namna ya kutumia mbolea na kwa wakati upi.

Ng'ondya ameeleza kuwa mbolea nikirutubisho au mchanganyiko wa virutubisho ambavyo mmea huhitaji ili iweze kuishi,kukua na kuzalisha hivyo ni vyema mkulima akatambua aina ya mbolea anayotumia na wakati gani anapaswa atumie.

"Nawakaribisha wananchi wote wa kanda ya kati na sehemu zingine zote kufika katika banda letu ili waweze kujifunza teknolojia mbalimbali kuhusu TFRA kama kanda ya kati tumekuja na mbolea za aina tofauti tofauti ili wakulima waweze kuziona na kujifunza kwasababu kuna mbolea za kupandia,kukuzia na mbolea kwajili ya Mbogamboga,"amesema.

Pamoja na hayo Ng'ondya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwakutoa ruzuku ya mbolea kitendo ambacho kitaenda kumnufaisha mkulima kutokana na mbolea kuwa bei kubwa na kupelekea wakulima kushindwa kumudu gharama hizo.


Aidha ametaja faida za kutumia mbolea zinadhibitiwa TFRA kuwa ni kuhakikishiwa ubora wa mbolea hizo na kumfanya mkulima kupata tija iliyokusudiwa kwasababu moja ya majukumu yao ya msingi ni kuzisajili hizo mbolea zote na mkulima anapata mbolea bora.

Kwa upande wake Afisa Udhibiti Ubora wa TFRA kanda ya kati Salvatory Kalokora amesema mtu yoyote haruhusiwi kufanya biashara ya mbolea bila kuwa na leseni.

Kalokora amesema ili kumruhusu mfanyabiashara kuuza mbolea TFRA imeanzisha mfumo wa kidigitali wa usajili wa wafanyabiashara wa mbolea.

Mamlaka ya udhibiti wa mbolea tanzania (TFRA) imeanzishwa kwa sheria ya mbolea na 9 ya mwaka 2009 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2014, pamoja na kanuni zake za mbolea za mwaka 2011 na marekebisho mwaka 2017 ambapo dhamira ya mamlaka hiyo ni kuhakikisha upatikanaji wa mbolea bora kwa wakulima wote kwa bei nafuu kwa ajili ya uzalishaji endelevu.
Kaimu meneja wa TFRA kanda ya kati, Joshua Ng'ondya akionesha aina mbalimbali za Mbolea.
Afisa Udhibiti Ubora wa Mbolea (TFRA), kanda ya kati salvatory Kalokora amesema mtu yeyote harusiwi kufanya biashara ya mbolea bila kuwa na Leseni.
Aina mbalimbali za Mbolea kutoka TFRA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...