Mkuu wa Bidhaa na Mauzo wa Benki ya NBC Bw.Abel Kaseko (katikati) Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza washindi wa kampeni ya “JAZA KIBUBU TUSEPE QATAR” mapema wiki hii . Pembeni yake kulia Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu, Bw.Elibariki SengaSenga kushoto ni Meneja Masoko wa Nbc Alina Kimaryo na mwishoni ni Mkuu wa kitengo cha Uhusiano Bw.Godwin Semunyu .Hafla ya hii ilifanyika makao makuu ya Benki ya NBC jjini Dar es salaam .

 Benki ya NBC yatangaza washindi wa “JAZA KIBUBU TUSEPE QATAR” siku ya Jumatano, Agosti 17, 2022. Ambapo kampeni hiyo ilianza Aprili mpaka mwezi wa September mwaka huu ikiwa na lengo la kutafuta washindi watakao hudhuria mechi za Kombe la Dunia linalotarajiwa kuanza mwezi Novemba mwaka huu, nchini Qatar. Mkuu wa bidhaa na Mauzo wa Benki ya NBC , Bwn.Abel Kaseko, akizungumza katika droo iliyofanyika kutafuta washindi wa shindano hilo, alisema walipanga kutafuta washindi hao mwezi wa tisa,lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao ambazo wamepewa na FIFA, imewabidi watafute washindi kabla ya tarehe 20 Agosti, 2022. 

“Washindi watakuwa ni wanne na Benki ya NBC itagharamia usafiri wa kutoka hapa kwenda Qatar, malazi na gharama zote zitakazohusika katika safari yote huko Qatar” Alisema. Akiwataja washindi hao, ambao ni Bw. Abdallah Tangarisi (Singida), Victor George Mwaifunga (Dar es salaam), Konolia Leonard Hinju( Songea) na Mpoki Wamakimbika(Mbeya).Aliongeza kuwa, Washindi hawa wanatarajiwa kuondoka nchini mwezi Novemba mwaka huu, kuelekea nchini Qatar. Mwisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...