Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazrui amesema wataendelea kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya maendeleo ili kuimarisha sekta ya afya nchini.
Akizungumza na washirika wa maendeleo ya afya D,Tree huko Ofisini kwake Mnzimmoja mara baada ya kufika na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu wahudumu wa Afya ya kujitolea (CHV), amesema wahudumu hao ni muhimu sana kwani wanaisaidia Wizara katika kuendesha harakati mbalimbali za Kiafya.
Amesema wahudumu wa afya wa kujitolea (CHV ) wanafanya kazi ngumu na kubwa katika jamii ikiwemo kuwapatia elimu ya kuimarisha Afya ya mama na mtoto jambo linaloisaidia Wizara katika kupunguza madhara yatokanayo na uzazi.
Aidha amefahamisha kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha kuwa inaimarisha maslahi ya wahudumu hao ili kuwapa moyo Zaidi wa kuendelea kufanya kazi na kuhakikisha Afya za jamii zinaimarika .
“Baadhi ya wanajamii hawana uwelewa kuhusu maendeleo ya afya ya uzazi ambapo mama mjamzito huchelewa kufika hospitali na kusababisha ongezeko la vifo vya mama na mtoto,hivyo wahudumu hawa wanajukumu kubwa la kutoa elimu zaid kwa jamii.”alisema Waziri Mazrui
Nao wajumbe wa Shirika la D,Tree wameishukuru Wizara ya afya kwa ushirikiano wao na kuahidi kuongeza ushirikiano Zaidi katika sekta hiyo ili kupambana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza . Wakati huohuo Waziri Mazrui alikutana na ujumbe kutoka Uturuki na kujadili kuhusu upatikanaji wa madawa na vifaa tiba ambavyo vitasaidia katika matibabu mbalimbali kwa wagonjwa.
Home
HABARI
WAZIRI WA AFYA AFANYA MAZUNGUMZO NA WADAU MBALIMBALI WA AFYA KATIKA KUIMARISHA SEKTA HIYO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...