Mkurugenzi Mtendaji wa Wentworth Reseurces Plc Katherine Roe akizungumza leo Agosti 4,2022 wakati wa uzinduzi wa ripoti ya kampuni hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambako pia kunafanyika kongamano la Nishati Tanzania.
Baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Wentworth Gas Ltd wakiwa makini kufuatia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Katherine Roe wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo.



Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMPUNI ya Wentworth Gas Ltd imezindua ripoti yake ya Mipango Endelevu ya mwaka 2021 inayochagiza ripoti kuu ya kampuni hiyo ya Wentworth Resources Plc inayotoa maelezo zaidi kuhusu utendaji na masuala muhimu ya mazingira , kijamii na utawala.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika leo Agosti 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Wentworth Reseurces Plc Katherine Roe amesema ripoti hiyo inafuatia muundo uliowekwa na bodi ya usimamizi ya viwango vya mipango endelevu na kuthibitishwa na mshauri wa kujitegemea aitwaye GHD Services Incorporated.

“Ripoti hii inaeleza mtazamo wa Wentworth wa uendelevu kupitia mkakati wa endelevu unaowiana na malengo ya maendeleo endelevu ya kimataifa unaozingatia nguzo tano za kimataifa.

“Nguzo hizo ni kusaidia mpito wa nishati unaowajibika, kuwezesha mabadiliko ya nishati, kujenga nguvu kazi mbalimbali na za kijumuishi, kuendeleza ukuaji kupitia ushirikiano na utawala thabiti wa mazingira , kijamii na utawala,”amesema.

Aidha amesema kwa kusambaza gesi asilia yenye kiwango cha chini cha kaboni kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na matumizi ya viwandani, Wentworth inachangia mageuzi ya nishati ya Tanzania kwa kuwezesha umeme wa bei nafuu nchini pamoja na uwekezaji katika miradi ya elimu,afya na maendeleo ya kitamaduni.“Kampuni yetu inatoa mabadiliko chanya ya kijamii.”

Ameongeza Wentworth inaendelea kupunguza uzalishaji wake wa kaboni baada ya kupata mojawapo ya viwango vya chini vya kaboni kwa mlango wa kila pipa la mafuta katika sekta ya mafuta na gesi ukilinganisha na kampuni yenye ukubwa kama wao yaliyoorodheshwa kwenye soko dogo la hisa Londan.

Roe amesema Wentworth imetangaza ushirikiano wa makubaliano kupitia ubia wa muda mrefu na kampuni ya Vitol ili kuendeleza miradi inayolenga jamii ambayo inatoa manufaa yanayolingana na malengo ya maendeleo endelevu kwa jamii ndani ya Tanzania.

“Wentworth ni kampuni inayojitegemea iliyoorodheshwa katika soko dogo la hisa London na mshirika katika washirika wa Mnazi Bay pamoja na TPDC,Maurel$Prom.Maelezo zaidi ya ripoti hii yanapatikana katika ripoti yetu ya mipango endelevu ya mwaka 2021.

“Kupitia historia yetu mahiri , mtindo thabiti wa biashara na ufanisi mkubwa wa kifedha Wentworth inazalisha gesi ili kuivusha Tanzania katika uchumi wa kesho.

“Ninafuraha kuthibitisha kwamba Wentworth Resource PLC inaunga mkono kakuni 10 za umoja wa mkataba wa kimataifa kuhusu haki za binadamu,kazi, mazingira na kupambana na rushwa.”amesema na kuongeza wamejitolea kuzifuata kanuni hizo za umoja wa mataifa na kuwa sehemu ya mkakati, utamaduni na shughuli za kila siku za kampuni yao.

Ameongeza pia wanashirikiana na Serikali ya Tanzania kuunga mkono agenda yake ya maendeleo ya taifa katika nishati na mazingira.“Kwa kufanya hivyo tunaboresha maisha ya watu.”
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Katherine Roe(katikati) akijadiliana jambo na sehemu ya maofisa wa kampuni hiyo baada ya kuzindua ripoti yake ya Mipango Endelevu mwaka 2021.
Maofisa kutoka Wentworth wakiwa katika meza kuu wakati wa uzinduzi wa ripoti ya kampuni hiyo inayohusu Mipango Endelevu 2021


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...