Na. Peter Haule, WFM, Singida
Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo, amewataka wataalam wa Idara na Vitengo vya Wizara hiyo kuhakikisha wanapitia kwa umakini mtiririko wa hatua za utekelezaji wa majukumu ya Wizara na kuuboresha ili uweze kuleta tija katika utoaji huduma bora na kwa wakati kwa manufaa ya Taifa.
Rai hiyo imetolewa mkoani Singida wakati akizungumza na timu ya wataalam wa wizara hiyo ambayo inapitia mtiririko wa hatua za utekelezaji wa majukumu na kuuboresha ili uweze kuwa na ufanisi.
Alisema kuwa ni vema Wizara ya Fedha na Mipango ikaonesha mfano wa kiutendaji wenye tija katika masuala ya mipango, uchumi, sera na usimamizi wa fedha na kuondoa utaratibu ambao haunatija kwa wizara, Taifa na wananchi kwa ujumla.
Alisema wizara hiyo inapofanyakazi kwa ufanisi inachochea maendeleo ya kiuchumi katika sekta nyingine na kutimiza lengo la Serikali la kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa.

Mkurugenzi wa Idara ya Mipango ya Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Moses Dulle, akielezea jambo wakati wa kikao kazi cha kuboresha mtiririko wa hatua za utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo, kinachofanyika mkoani Singida.

Baadhi ya Washiriki wa kikao kazi cha kuboresha mtiririko wa hatua za utekelezaji wa majukumu ya Wizara, kinachofanyika mkoani Singida.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (WFM) Singida)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...