Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Klabu ya Yanga imeendelea kufanya mabadiliko ya uongozi baada ya Rais wa Klabu hiyo kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji, kumteua Saad Kawemba kuwa Mkurugenzi wa Mashindano, na kumteua Walter Harson kuwa Meneja mpya wa Kikosi hicho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu hiyo, Saad Kawemba anapewa majukumu hayo baada ya aliyekuwa kwenye nafasi hiyo, Thabith Kandoro kumaliza mkataba wake ndani ya Klabu hiyo.
Walter Harson anakuwa Meneja wa timu hiyo ya Wananchi, akichukua nafasi ya Hafidh Saleh ambaye amepangiwa majukumu mengine ya kuwa Mratibu wa Timu. Uteuzi huo unaanza rasmi Agosti 1, 2022.
Hata hivyo, Yanga SC itazindua rasmi Wiki ya Mwananchi mapema, Agosti 1, 2022, kuelekea Siku ya Mwananchi, tayari Yanga SC wameunda Kamati yenye Wajumbe Saba wakiongozwa na Mwenyekiti Arafat Haji ambaye ni Makamu wa Rais wa Klabu hiyo.
Wajumbe hao ni Wakili Simon Patrick, CPA. Haji Mfikirwa, Taji Liundi, QS. Said Yassin Mrisho, Khamis Abeid Dacota na Christinah Oscar Korosso. Kilele cha Wiki ya Mwananchi kinatarajiwa kuwa Jumamosi ya Agosti 6, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Meneja mpya wa Klabu ya Yanga, Walter Harson (pichani), Walter amewahi pia kuhudumu nafasi mbalimbali katika Klabu ya KMC ikiwemo nafasi ya Katibu Mkuu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...