Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo kushoto akiwa na Mkurugenzi wa Biashara wa Azania Group, Joel Laiser wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ngano wenye chapa ya Azania Premium Home Flour (PHF) jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo akizungumza wakati wa uzinduzi wa ngano wenye chapa ya Azania Premium Home Flour (PHF) jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2022.
Mkurugenzi wa Biashara wa Azania Group, Joel Laiser akizungumza wakati wa uzinduzi wa ngano wenye chapa ya Azania Premium Home Flour (PHF) jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2022.
Mkurugenzi wa Biashara wa Azania Group, Joel Laiser akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa wakati wa uzinduzi wa ngano wenye chapa ya Azania Premium Home Flour (PHF) jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2022.
Mama Lishe Maria Mbago akielezea namna ambavyo bidhaa mpya ya Unga wa ngano wa Azania PHF jinsi unavyo mrahisishia kazi wakati akitengeneza vitafunwa mbalimbali.

*Dc Jokate ataja kuwa wakazi wa Temeke hufanya kazi na Azania Group
*Apongeza kwa kusaidia mama lishe baba lishe

Na Mwandishi wetu Michuzi TV
MKUU wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo amesema kuwa Azania Group imeajiri idadi kubwa ya wafanyakazi kutoka katika wilaya ya Temeke hivyo amewaasa waendelee kuhudumia wananchi hasa akina mama ambao ndio wanufaika wakubwa.

Ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa unga wa ngano wenye chapa ya Azania Premium Home Flour (PHF) jijini Dar es Salaam leo Septemba 29, 2022. Amesema kuwa kwa kuwa Azania Group wanabidhaa bidhaa nyingi zaidi kama vile mafuta ya kupikia, bidhaa ya nazi anatumaini kuwa wata ziboresha ili kumletea urahisi Mama Lishe,wanawake na wanaume katika upatikanaji wa chakula bora na chenye manufaa kwa wanaTemeke na Tanzania kwa Ujumla.

“Niwapongeze kwa kazi kubwa na mchango mkubwa wanaoutoa katika upatikanaji wa bidhaa za chakula na uthibitisho wake ni baada ya ujio wa bidhaa yao mpya ya Unga wa Ngano kwa ajili ya kupikia vitu mbalimbali kama vitafunwa na kurahisisha huduma na kazi za upishi kwa watumiaji hususani kwa mama zangu ambao ni Mama lishe lakini pia wanufaika(walaji).” Amesema DC Jokate

Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Biashara wa Azania Group, Joel Laiser ametaja sifa za unga huo kuwa ni mweupe, laini na wenye kudumu kwa matumizi ya muda mrefu na kukidhi aina mbalimbali za mapishi.

"Unga wetu mpya wa Azania PHF unakuja kama sehemu ya utafiti uliofanywa na kugundua uhitaji wake hivyo ili kuleta suluhu na kuleta utofauti kwenye soko na urahisi kwa watumiaji, Azania tumeona kuwa ni vyema kuja na bidhaa hii kwani mara nyingi watu wengi wanabanwa sana na muda na kushindwa kuzalisha bidhaa zenye ubora kama vile Maandazi, Chapati na vitafunwa, bidhaa yetu hii itatoa nafasi ya kuzalisha vitafunwa vingi zaidi kuliko vile vilivyozoeleka.” Amesema Joel Laiser

Akiendelea kutaja sifa za unga huo wa ngano amesema Mvuto wa chakula chochote kile unatokana na muonekano wake na ladha ya chakula husika. lengo lao katika uzinduzi wa bidhaa hiyo ni kuongeza faida na kuongeza thamani kwa wateja wao.

“Tunaamini soko letu liko tayari kusambaza bidhaa hii bora kabisa ambayo watumiaji wake watagundua kuwa imetengenezwa kwa ubora na imewekwa viungo vyenye ladha ya hali ya juu."

“Unga wa Azania PHF utapatikana katika maduka yote Tanzania na yaliyopo mipakani, Sisi kama Azania group tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutoa bidhaa bora, zenye suluhu za huduma kwa watumiaji wetu.” Amesema Laizer

Mama Lishe Maria Mbago ameeleza kuwa mara ya kwanza kutumia bidhaa mpya ya Unga wa Azania PHF ambao ni mweupe na laini kuliko unga mwingine.

“Unanipa nafasi mimi mpishi kupika haraka zaidi maana ni laini sana na unatoa vitafunio laini na vitamu na vyenye ladha natarajia kuwa bidhaa hii mpya ya Unga wa ngano itanisaidia zaidi kuongeza wateja kutokana na ubora utakaotokana na vitafunwa nitakavyotengeneza kupitia unga huu." Amesema Maria

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...