
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitoa mkono wa pole kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.) ametoa pole kwa Familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi kufuatia kifo cha mtoto wake Hassan Ali Hassan kilichotokea tarehe 31 Agosti, 2022 katika Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja, Zanzibar.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...