BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele mapema leo tarehe 13/09/2022 amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Indonesia Mhe. Joko Widodo katika hafla iliyofanyika kwenye Kasri la Merdeka jijini Jakarta.
Katika hafla hiyo, wawili hao walipata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji.
Hatua hiyo ya Mhe. Balozi Makocha Tembele kuwasilisha hati zake za utambulisho inaashiria kuanza rasmi kwa utumishi wake katika nchi hiyo.
.jpg)
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Joko Widodo
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akisalimiana na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Joko Widodo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...