BARAZA la Maadili lipo Kwenye uchunguzi wa Malalamiko tisa toka sehemu mbalimbali, uchunguzi huo umeanza Septemba 6 na utatamatika Septemba 16 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Kamishina wa Maadili Jaji Sivangilwa Mwangesi wakati akizungumza na wahandiishi wa habari jijini Dodoma.

Mwangesi amesema kamishina wa maadili ndiye anayepokea malalamiko toka sehemu tofauti tofauti na kuaza uchunguzi wa malalamiko hayo na baadae kuwakilisha malalamiko hayo kwenye balaza la maadili.

" Mpaka sasa kuna malalamiko tisa ambayo yanachunguzwa na baraza la maadili baada ya uchunguzi huo baraza litaandaa maoni yake kutokana na lalamiko lililotolewa na ushahidi ambao umepokelewa , uchunguzi huu unafanyika kwa mujibu wa kifungu cha 25(5)na 296 cha sheria ya maadili ya uongozi wa umma ( sura 398)" amesema Mwangesi.

Pia amesema baraza halitakuwa na siku ya kutoa hukumu bali litachukua uamuzi wake kulingana na sheria ilivyo na litatoa ushauri baada ya hapo anakabidhiwa kamishina wa maadili kwa ajili ya kupeleka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema jukumu kubwa ya taasisi hiyo ni kuchunguza tabia ya mwenendo wa kiongozi wa umma yoyote kwa madhumuni ya kuhakikisha masharti ya sheria ya maadili ya uongozi ya umma yanazingatiwa .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...