Katika kufanikisha azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha na kurahisisha malipo nchini, Benki ya CRDB imeingia mkataba wa makubaliano na kampuni ya huduma za malipo ya Selcom utakao wezesha wateja wa kampuni hizo kufanya na kupokea malipo kwa urahisi.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB, Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile alisema ushirikiano huo utawawezesha wateja kufanya malipo kwenye huduma ya SelcomPay kupitia njia ya kidijitali ya malipo ya SimBanking kwa urahisi zaidi.

“Kupitia ushirikiano huu wateja wa Benki sasa wataweza kufanya malipo katika maeneo ya biashara/mifumo(application za simu au websites) zinayopokea malipo kupitia Selcom kwa kutumia QR Code na Lipa Namba za Selcom kutumia SimBanking App au ile USSD kwa kupiga *150*03#…” alisema Mwile.

Mwile alibainisha kuwa hatua hiyo pia itawawezesha wafanyabiashara wengi nchini kupata urahisi wa kupokea malipo hasa kwa kuzingatia kuwa Benki ya CRDB na Selcom zina mtandao mpana, na tayari zimeweza kuunganisha biashara nyingi katika mifumo yao ya upokeaji malipo ya SimBanking na SelcomPay.

Aidha, hafla hiyo ya utiaji saini mkataba wa makubaliano imeenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya elimu kwa wateja yenye kauli mbiu ya “UKIONA SELCOM LIPA! UKIONA CRDB LIPA!” ikiwa na lengo kuelimisha wateja namna ambavyo wanaweza kutumia vizuri fursa hiyo ya ushirikiano baina ya Benki ya CRDB na Selcom kukamilisha malipo yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom alinukuliwa akisema "Ushirikiano huu kati ya Selcom na Benki ya CRDB ni uthibitisho tosha wa dhamira ya taasisi hizi mbili ya kumpa kipaumbele mteja. Zikiwa taasisi mbili kubwa katika kutoa huduma za kifedha na zile za kiteknolojia ya malipo, Selcom na CRDB waliona umuhimu wa kumrahisishia mteja njia ya kulipia huduma na bidhaa mbalimbali kwa kutumia simu yake ya mkononi moja kwa moja kutoka kwenye akaunti yake ya CRDB. Hii pia inawawezesha wafanyabiashara wanaotumia huduma za Selcom kuweza kuongeza wigo wa kupokea malipo"

Ndugu Sameer hakusita kuonesha matumaini yake kwamba hatua hii ya ushirikiano wa kiteknolojia itaongeza watumiaji wa huduma za malipo mitandaoni, kupunguza gharama za kutumia huduma za malipo na pia kuongeza wigo wa Ujumuishwaji wa Kifedha katika Jamii.”

Ushirikiano huu mpya baina ya Benki ya CRDB na Selcom unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika huduma za malipo nchini. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa inaonyesha Benki ya CRDB ina vituo vya malipo zaidi ya 20,000, wakati Selcom ina vituo vya malipo zaidi ya 80,000. Kwa pamoja taasisi hizo pia zinaangazia kuongeza vituo vya malipo ili kusogeza huduma kwa wananchi wengi zaidi.






Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka Selcom, Geofrey Mwakamyanda (wa kwanza kushoto) kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom, Sameer Hirji, akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wakizindua ushirikiano wao mpya na CRDB katika kufanya miamala ya fedha kwa lengo la kupanua wigo wa huduma za kifedha na kurahisisha malipo nchini. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa wateja binafsi na wa biashara wa CRDB Bonaventura Paul na wa mwisho kulia ni Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa CRDB Bruce Mwile.



Kaimu Mkurugenzi wa wateja binafsi na wa kibiashara wa CRDB, Bonaventura Paul (aliyesimama katikati) akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wao na Selcom.

CRDB na Selcom wakipeana mikono kwenye hafla ya kusherehekea uzinduzi wa ushirikiano wao wa kurahisisha malipo ya simu kupitia CRDB and Selcom.


Baadhi ya wahudhuriaji katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano kati ya CRDB na Selcom iliyofanyika Makao Makuu ya CRDB Septemba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...