TAASISI ya Kijamii ya BIBI Trust ya Mjini Bukoba imedhamini Ligi ndogo ya mpira wa miguu ya Kombe la BIBI Cup 2022 katika Kijiji cha Rwanda Kata ya Ibuga Kamachumu mkoani Kagera.
Ligi hiyo ilianza Agosti 20 mwaka huu kwa kushirikisha Vitongoji vinne katika Vijiji vya Busingo A, Busingo B, Kitunga-Kyamawa na Bunene-Butundu na kuhitimishwa Septemba 4 2022 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ruzinga iliyopo Kamachumu.
Ligi hiyo ya Bibi Cup 2022 imeitimishwa kwa mechi kati ya timu ya Kitunga-Kyamawa na Busingo B na matokeo ya mchezo huo ni sare ya bao 2-2.
Mshindi wa ligi hiyo ni Bunene-Butundu ambayo imebeba Kombe, jezi 11, mpira mmoja na fedha tasilimu sh 50000, mshindi wa pili ni Kitunga-Kyamawa, jezi 11mpira na fedha Sh 25000.
Ligi hiyo imeanzishwa na wajukuu wa Bibi Yustina Kokugonza aliyefariki dunia 2018 ikiwa na lengo la kumuenzi bibi yao kwa namna alivyokuwa akiishi na jamii na familia kupenda kwaweka pamoja bila kujali uwezo wao wala itikadi za kidini au za vyama katika suala la kuleta maendeleo.

Wachezaji wa timu ya Bunene-Butundu wakiwa na wamebeba kombe baada ya kuwa mabingwa wa ligi ya BIBI Cup 2022.

2. Mkurugenzi wa Taasisi ya BIBI Trust, Teddy Rweyendera, akizungumza kabla ya kukabidhi Kombe kwa mshindi wa ligi ya BIBI Cup 2022 timu ya Bunene-Butundu baada ya mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ruzinga, Kamachumu mkoani Kagera juzi.

Naodha wa timu ya Kitunga-Kyamawa, Albert Alexander akiambatana na Naodha Msaidizi, Method Melchades.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...