Na Abdullatif Yunus Michuzi TV Kagera

Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Bukoba Developers (BUDES) kwa Kushirikiana Shirika la Management Development for Health (MDH) wameungana pamoja ili kuongeza nguvu ya utoaji elimu juu ya chanjo ya Uvico19, pamoja na magonjwa mengine ya mlipuko lengo likiwa ni kuendelea kuhamasisha Jamii juu ya umuhimu wa Chanjo hiyo.

Akizungumza katika Semina elekezi Mkurugenzi wa BUDES ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Wakili Stephen Byabato(NWN) amesema Taasisi hiyo Yenye Makao Makuu Bukoba Manispaa, imelenga zaidi kusaidia katika Mambo ya Kijamii yakiwemo masuala ya Utunzaji Mazingira, Elimu, Afya, Uchumi na Msaada wa kisheria.

Kupitia Mafunzo hayo yaliyoandaliwa Maalum kwa viongozi wa mitaa na kata kumi na nne, wakiwemo Wenyeviti wa Serikali za mitaa, Watendaji wa kata na mitaa pamoja na Madiwani wa Manispaa ya Bukoba, Byabato ameongeza kuwa MDH na BUDES wameamua kuungana na kutoa mafunzo hayo kwa viongozi hao kwa lengo la kuendelea kutoa elimu na hamasa ya chanjo ya uvico19 Wilaya ya Bukoba Mjini, huku BUDES wakiwa Tayari kutoa Vijana 14 watakaosaidiana na MDH kutoa Elimu.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika Mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Albert Chalamila amesema bado Mkoa wa Kagera mwitikio wa wananchi kuchanja ni mdogo na hivyo viongozi wanao wajibu wa kuendelea kutoa hamasa kwa jamii ili waelewe lengo la serikali kuleta chanjo na umuhimu wake

"Ndugu zangu Serikali inayo nia ya dhati ya kuwakinga wananchi wake dhidi ya ugonjwa wa Uvico19 hivyo haiwezi kuleta chanjo inayodhuru watu wake."

Mafunzo hayo yameambatana na Shughuli ya kukabidhi Pikipiki 76 kwa wahudumu wa afya, zenye thamani ya shilingi milioni Mia mbili na ishirini zilizotolewa na MDH kwa kushirikiana na BUDES ambazo zitasaidia watoa huduma za afya kutoa elimu kwa jamii.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...