Mtaalam wa Mahusiano wa BUNI -Costech, Promise Mwakale akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi juu ya Mafunzo ya vijana wabunifu wa kiteknolojia kutoka kwenye vyuo mbalimbali nchini.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Buni Talent wakifuatilia wenzao waliokuwa wakiwasilisha mawazo yao ya Kibunifu ya Kiteknolojia leo Septemba 9,2022 mkoani Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja.

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), imefunga programu yake ya kuibua vijana wenye vipaji kutoka vyuo vikuu, inayofahamika kwa jina la Buni Talent Hub,kwa mwaka 2022.Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza wakati wa ufungaji mafunzo hayo, leo Ijumaa, Septemba 9, 2022, jijini Dar es Salaam, Mtaalamu wa Mahusiano wa Kumbi ya Ubunifu ya Buni Hub, Promise Mwakale, amesema program hiyo iliyoanza Julai hadi Septemba mwaka huu, ilichukua wanafunzi 42 kutoka vyuo vikuu vinne.

Vyuo hivyo ni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Taasisi ya Uhasibu (TIA) na Chuo cha Ardhi.

Mwakale amesema, kupitia program hiyo, vijana hao wamefanikiwa kuandaa bunifu mbalimbali ambazo waliziwasilisha kwa jamii ili kuona kama zinatija kwa ajili ya kuzibadilisha kuwa bidhaa au huduma.

“Leo tunamaliza program ya Talent Hub ambayo vijana 42 wanahitimu, wanamaliza mafunzo ya wiki kumi yaliyoanza toka Julai hapa COSTESH. Wamepitia kuangalia mawazo yao, kutengeneza timi, wakabadilishana mawazo kwa ajili ya kuyaweka vizuri,” amesema Mwakale.

Amesema, program hiyo kwa sasa ina mwaka wa saba na kwamba imesaidia vijana wengi kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

Mhitimu wa programu hiyo, Ibrahim Laseko, amesema imewapa nafasi ya kujifunza kuandaa wazo kutokana na changamoto zinazoikabili jamii, ambapo kikundi chake kimeanzisha mtandao unaofahamika kwa jina la Kazi Faster, ambao huwakutanisha waajiri na watu wanaotafuta kazi.

“Tuliumba wazo, na kwa sasa Application tunayoifanyia kazi inaitwa Kazi Faster, kwa sasa haijakamilika ila itakuwa App ndani ya muda mchahe na tumelenga watumiaji watakuwa vijana ambao wenye uwezo wa kuingia kwenye mtandao kufanya kazi mbalimbali ili kujipatia kipato hii itasaidia kuondokana na watu kukaa vijiweni na kusikilizia kazi ambazo hazipo,” amesema Laseko, ambaye ni mhitimu wa Taasisi ya Uhasibu (TIA).

Mhitimu mwingine wa programu hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Teddy Micky, amesema “Programu ya Buni tunatapa nafasi ya kujua jinsi gani tunaweza endeleza au kuanzisha biashara au kuandaa kitu kipya kwa ajili ya jamii yetu. Tumejifunza jinsi gani tunaweza fanya biashara au kitu ninachotaka kuanzisha kwenye sayansi na teknolojia.”

Teddy amesema, katika kundi lake lililotokana na programu hiyo, wamefanikiwa kuanzisha mtandao ‘Application’ inayopatikana katika simu za kiganjani, kwa ajili ya kuwakutanisha wagonjwa na madaktari.

“Mimi na kundi langu tumeweza kuanzisha App ambayo itasaidia mgonjwa kumuita daktari nyumbani na kupata huduma hapo alipo. Lakini pia tumepata kujua vitu mbalimbali katika jamii hasa kwa kuangalia maisha halisi ya Watanzania na kutatua changamoto za kila siku katika jamii yetu.” Amesema Teddy.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...