Na Mwandishi Wetu, Chato

MBUNGE wa Jimbo la Chato mkoani Geita Dk. Merdard Kalemani amemshukuru Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo mkoani Geita ikiwemo katika jimbo hilo.

Dk. Kalemani ameyasema hayo leo Septemba 3, 2022 wakati wa mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana ambaye amewasili mkoani Geita kwa ajili ya ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uachaguzi ya CCM na kupokelewa katika eneo la Nyarutembo, wilayani Chato.

“Kwanza kabisa jambo kubwa ambalo tunapongeza kwa miaka mitatu iliyopita Chama kilitoa sh. milioni 32 kwa ajili ya kujenga ofisi za CCM za wilaya ya Chato, hivyo tunashukuru sana. Tunaomba tufikishie shukrani nyingi kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan, tunampongeza na tupo pamoja naye, hivyo atembee kifua mbele.

“Makamu Mwenyekiti (Kinana) hapa upo Nyarutembo, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imefanya mambo mengi, katika kipindi cha miezi takribani 18 tumepokea takribani sh. bilioni 47 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, tunamshukuru sana Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na viongozi wengine, tumepata fedha sh. bilioni 2.5 kwa ajili ya miradi ya barabara zinazosimamiwa na TARURA, zimeshajengwa bado kilomita 17 kati ya kilomita 48.

“Tumepewa Sh. bilioni 8 kwa ajili ya vituo vya afya ambapo sasa vituo vinane vinajengwa, tumeshajenga vituo vya afya takribani 16 katika kata 23, tufikishie shukrani kwa Rais wetu na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Rais Samia). Fedha ya UVIKO-19 tulipata nyingi mwaka uliopita kwani tulipata Sh. bilioni 3.47 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 183, yote yamekamilika na wanafunzi wanasoma.

“Katika miradi ya maji, kupitia mradi wa miji 28 tulitupa Sh. bilioni 30.2, tunampongeza Rais Samia kwa kutuoa fedha hizo, hapa kero kubwa kama unavyoona ni maji, lakini Rais Samia ametatua…maji yanakuja na hapa muda sio mrefu.” amesema.

Dk. Kalemani amempongeza Makamu Mwenyekiti Kinana kwa kufika mkoani humo kukagua uhai wa Cahama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kumuomba awafikishie salamu za shukrani kwa Rais Samia kwani aliahidi miradi yote iliyopo Chato itakamilika na ametenda, ametekeleza na fedha zinaendelea kumiminika.

“Miezi miwili iliyopita tumepokea Sh. bilioni 17 kwa ajili ya miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa Chato,” amesema Dk. Kalemani mbele ya Kinana ambaye ameambata na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka.

Kinana ambaye ameongozana na Shaka amehitimisha ziara yake mkoani Kagera na kuwasilie leo Septemba 3,2022 mkoani Geita kuendelea na ziara hiyo yenye lengo la kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akimtambulisha Mbunge wa jimbo la Chato Dkt Medard Kalemani kwa Wana CCM na baadhi ya Wananchi waliofika kuulaki ugeni huo katika  kijiji cha Nyarutembo wilayani Chato mkoa wa Geita akitokea mkoani Kagera .Kinana ambaye ameongozana na Shaka amehitimisha ziara yake mkoani Kagera na kuwasilie leo Septemba 3,2022 mkoani Geita kuendelea na ziara hiyo yenye lengo la kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.
Ni Shangwe tuu Chato : Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na Katibu wa NEC Itikazi na Uenezi CCM Taifa Shaka Hamdu Shaka na wana CCM wengine wakifurahia jambo baada ya mapokezi na utambulisho katika kijiji cha Nyarutembo wilayani Chato mkoa wa Geita akitokea mkoani Kagera kuendelea na ziara yake.
Katibu wa NEC Itikazi na Uenezi CCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiteta jambo na MKuu wa MKoa wa Geita Mhe.Martine Shigela mara baada ya kupokewa leo Septemba 3,2022 katika kijiji cha Nyarutembo wilayani Chato mkoa wa Geita akitokea mkoani Kagera  akiwa ameambatana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana ,pichani kati ni Mbunge wa Chato Dkt Medard Kalemani
MKuu wa MKoawa Geita Mhe.Martine Shigela  akiwasalimia baadhi ya wana CCM pamoja na baadhi ya Wananchi  mara baada ya kutambulishwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita Said Kalidushi akizungumza mbele ya Wanachama wa chama hicho  mara baada ya kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikazi na Uenezi CCM Taifa Shaka Hamdu Shaka,leo Septemba 3,2022 katika  kijiji cha Nyarutembo wilayani Chato mkoa wa Geita akitokea mkoani Kagera kuendelea na ziara yake. Pichani kulia ni MKuu wa MKoa wa Geita Mhe.Martine Shigela akiwa na Mbunge wa jimbo la Chato Dkt Medard Kalemani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...