Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia bidhaa na vifaa vya matumizi ya aina mbalimbali katika mabanda ya Maonesho kwenye kilele cha Tamasha hilo la siku ya Kizimkazi tarehe 03 Septemba, 2022
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na mke wa Rais
wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi mara baada ya kuwasili katika eneo la
Kizimkazi Dimbani kwa ajili ya kushiriki kwenye Tamasha la Kizimkazi
tarehe 03 Septemba, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kuhusu matumizi ya vifaa mbalimbali vya Uvuvi kutoka kwa Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar KMKM wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho kwenye Tamasha la siku ya Kizimkazi tarehe 03 Septemba, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Kiazi Kikuu kilichochimbuliwa kwenye ardhi kavu na Wazee wa Jadi kutoka Kikundi cha Shomoo cha Kizimkazi katika Siku ya kilele cha Tamasha hilo lililofanyika Kizimkazi Dimbani tarehe 03 Septemba, 2022
Wataalam wa Jadi wa Kikundi cha Shomoo cha Kizimkazi wakionesha uwezo wa kufanya vitu mbalimbali wakati wa Sherehe za Tamasha hilo lililofanyika Kizimkazi Dimbani, Zanzibar tarehe 03 Septemba, 2022.
Wasanii wa Kikundi cha Zanzibar One wakitoa burudani kwenye Tamasha hilo la Kizimkazi lililofanyika Kizimkazi Dimbani, Zanzibar tarehe 03 Septemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wageni mbalimbali wakati wa kilele cha Tamasha la Kizimkazi lillilofanyika Kizimkazi Dimbani tarehe 03 Septemba, 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...