Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali mstaafu Abdulrhaman kinana amemshauri mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigella kuangalia namna nzuri ya kuupanga mji wa Geita uwe na Muonekano mzuri na wa kisasa na si ulivyo kwa Sasa.

Kinana amebainisha hayo leo September 4,2022 Mjini Geita wakati wa ziara yake ya Siku moja inayolenga kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuangalia Uhai wa Chama hicho.

Kinana amesema Geita ni mkoa mpya ambao una maeneo mengi, hivyo ni muhimu kwa viongozi kuanzia ngazi ya maafisa mipango kuangalia namna nzuri na bora ya kuupangilia ili uwe miongoni mwa miji mizuri na inayovutia hapa nchini.

"Geita inayo Miradi Mingi ya Ki-maendeleo ambayo inatekelezwa ikiwemo Ofisi za Serikali na Idara zake, Makazi ya Watumishi wa Umma pamoja na Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo hivyo ni muhimu kwa Mamlaka za mkoa huo kuweka mikakati ya kuhakikisha Suala la Mipango miji linazingatiwa ili kuupa hadhi na muonekano mzuri" amesema Kinana.

Akiwa Geita Komredi Kinana amekagua Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo ambao unagharimu Bilioni 20.1, Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita ambapo Ujenzi wake umegharimu Shilingi Bilioni 7.75 pamoja na Uwanja wa Mpira wa Miguu unaomilikiwa na Halmashauri ya mji wa Geita.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akikagua baadhi ya majengo likiwemo la mama na mtoto katika Hospitali ya Mkoa wa Geita leo Septemba 4,2022, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025. Wa pili kulia
ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Martine Shigella

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akikagua jengo la Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025. Kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Shaka Hamdu Shaka na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Martine Shigella
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana alifika kukagua jengo la Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Geita leo Septemba 2022, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Moja ya jengo ambalo ujenzi wake haujakamilika katika Hospitali ya Mkoa wa Geita,ambapo leo Septemba 4,2022 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana alifika kukagua baadhi ya, majengo katika hospitali hiyo akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...