Na Mwandishi wetu - Dodoma


WAKATI Tume ya haki za binadamu na utawala bora ikiadhimisha miaka 20 imeelezwa kuwa tume imefanikiwa kuratibu masuala ya haki za binadamu na utawala bora kama vile kudhibiti mauaji ya watu wenye ualbino, nakuhakikisha haki za binadamu zinazingatiwa kwenye sehemu zenye vizuizi kama vile magereza, mahabusu na vituo vyakulea watoto.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na waziri wa katiba na sheria Dkt Damas Ndumbaro wakati akifunga kilele Cha maadhimisho ya miaka 20 ya tume hiyo ambapo amesema imehjitahidi katika kuboresha na kusimamia haki za binadamu kwenye utendaji wao.

‘’ Tume imefanya mambo mengi na kama tunavyojua haki za binadamu zitaendelea kuwa kipaumbele kikubwa katika nchi yetu kwa kuhakikisha haki ya kila mwanandamu zinaendelea kutekelezwa’’ Amesema Dkt Ndumbaro.

Naye Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema Wakati tukiadhimisha miaka 20 hali ya haki za binadamu inaendelea kuimarika na hii inatokana na kauli za Rais ambazo amekuwa akizitoa kwa kukemea ukikwaji wa haki za binadamu.

Aidha ameipongeza serikali ya mapinduzi zanzibar kwakuwa mstari wa mbele katika kuimarisha utawala bora na kuondosha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

‘’Watumishi wote wa umma tuwaige viongozozi hawa kwa kutimiza majukumu yetu kwa kuzingatia haki za binadamu na tusibiri viongozi wakuu watoe kauli ndipo nanyi mnajitokeza’’ Amesema jaji Mwaimu

Aidha Jaji mwaimu ameongeza kuwa Tume imeendelea kufanya tafiti kuhusu hali ya haki za binadamu, kwa kipindi cha miaka 20 tume imekuwa ifuatilia chaguzi na kutoa mapendekezo.

Maadhimisho haya yamefikia kilele chake leo katika wiki ya maadhimisho yakiwa yameambatana na shughuli mbalimbali kama vile kuelimisha wananchi majukumu ya tume ilipotoka na ilipo kwa sasa.

Hata hivyo Maadhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo miaka 20 yakuhamasisha haki za binadamu na utawala bora kwamaendeleo ya nchi.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya  Tume ya Haki za binadamu na utawala bora jijini Dodoma leo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...