Na Eva Ngowi - Wizara ya Fedha na Mipango

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Emmanuel Tutuba amekutana na kufanya Mazungumzo na timu ya Taasisi ya TradeMark East Afrika (TMEA) leo jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na utambulisho wa Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa TMEA Bw. David Beer ambaye alianza kazi rasmi tarehe 01 mwezi Septemba 2022, na aliambatana na Afisa Mtendaji Mkuu aliyemaliza muda wake Bw.Frank Matsaert.

Akizungumza katika majadiliano hayo Bw. Tutuba alisema Taasisi ya TMEA ni wadau muhimu ambao tumekuwa tukifanya nao kazi muda mrefu, na kusema kuwa Shirika hili lilianzishwa mwaka 2010 kwa dhumuni la kufanya shughuli zake Afrika ikiwemo kuongeza wigo wa biashara ambayo imewezesha mashirika ya maendeleo ya nchi mbalimbali zikiwemo Belgium, Canada, Dernmark, European Union, Ufaransa, Finland, Ireland, Nertherlands, Norway, United Kigdom na United States of Amerika.

Bw. Tutuba alisema TMEA imetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kuwajengea uwezo wataalamu wa Serikali, kujenga baadhi ya vituo vya Pamoja vya forodha mipakani, kununua Scanner inayotumika katika mpaka wa Tunduma, Ukarabati wa Scanner inayotumika Bandari ya Dar es Salaam na wamefanya shughuli mbalimbali za kuhakikisha kwamba nchi inatekeleza Mkakati wa Kitaifa wa kujenga mazingira bora ya kufanyia biashara na kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara.

“Tumeongea mafanikio mengi ambayo wameyatekeleza na kwa ujumla tumefahamisha miradi waliyofanya, unajua hawa TMEA wametusaidia katika miradi mbalimbali ya kwenye vipaumbele walivyokuwa wanavitekeleza kwa ujumla kwa sababu vinaendana na mpango wa Maendeleo wa miaka mitano, lakini vilevile wanaendelea kutekeleza dira yetu ya maendeleo ya mwaka 2025 kwa upande wa Tanzania Bara lakini kwa Zanzibar kuna maeneo wamekuwa wakiyafanyia kazi yanayoendana pia na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2050” Alisema Bw. Tutuba

Aidha Bw.Tutuba alisema wameijulisha Taasisi hiyo kuwa kuna umuhimu wa kuendelea kushirikiana, na kwa wafadhili wote wanaochangia zile fedha wamewajulisha kwamba watazitumia vizuri. Pia Bw. Tututba alimkaribisha Mtendaji huyo mpya wa Taasihi yo Bw. David Beer na kumhakikishia kwamba Serikali inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wa maendeleo na kwamba Serikali iko mstari wa mbele kujenga mazingira wezeshi ya kuhakikisha shughuli zote za biashara zinafanyika vizuri.

“Tumewajulisha kwamba nchi yetu iko vizuri kiuchumi, kisiasa na hata shughuli mbalimbali za uwekezaji na kufanya gharama za uwekezaji kuwa chini maana yake wawekezaji wengi tunawakaribisha waje kuwekeza nchini na wakati huo huo sisi tunaendeleza kuimarisha miundombinu ambayo itawezesha utekelezaji wa shughuli zao vizuri” Alisema Tututa

Bw. Tutuba aliongeza kuwa katika majadiliano ya kuandaa awamu ya tatu ya mkakati wa utekelezaji wa pamoja ni kuweka nguvu kwenye miradi mikubwa na miradi mingine midogo midogo iliyokuwa inafanyika na kuangalia pale ilipofanikiwa iunganishwena kufanya mambo makubwa zaidi lakini pale ambapo bado kuna kuzitatua haraka changamoto zilizojitokeza.

“Kuhusu usawa wa kijinsia katika uongozi nikiwafahamisha kwamba sasa hivi ukiangalia Tanzania ni nchi pekee ambayo mihimili miwili inaongozwa na wanawake ikiwepo Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu lakini pia tunae Dkt Tulia Ackson Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni nchi pekee ambayo iko imara na imethibitisha kwamba wanawake wanaweza kuongoza vizuri na nimewataka waangalie namna ya kuwezesha shughuli za kibiashara kwa wanawake na vijana katika vipaumbele vya awamu inayokuja.”. Alisema Tutuba

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa TMEA Bw. David alisema ameanza majukumu yake hivi karibuni na Tanzania ni nchi yake ya kwanza kutembelea.

“Najivunia kuwa mwanafamilia wa Trade Mark na tuna historia ndefu na Serikali ya Tanzania hivyo tutaboresha biashara na kuvuka mipaka hasa kusafirisha bidhaa nje. Namshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Tutuba kwa kuchukua muda wake kuonana na uongozi wa Trade Mark kujadili sio tu mafanikio tuliyoyapata huko nyuma ni pamoja na ufanyaji kazi mzuri wa bandari ya Dar es Salaam na uwekaji wa kituo cha Pamoja Tunduma.” Alisema Bw. Beer.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TMEA aliyemaliza muda wake Bw. Frank alisema anaishukuru Tanzania kwa ushikiano waliounesha kwa kipindi cha miaka kumi na mbili ambayo tumefanya kazi pamoja kwani tumefanikiwa vya kutosha.

”Namtakia heri mrithi wangu; Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Tutuba asante sana maana kwa maneno mazuri uliyosema, unayo timu nzuri ambayo itafanya vizuri huko mbeleni. “Alisema Bw. Frank

Trade Mark ni Shirika ambalo lilianzishwa mwaka 2010 na Makao makuu yake yako Nairobi Kenya ambapo ofisi zake kwa Tanzania ziko Arusha na Dar es Salaam. Kwa sasa TMEA inaendelea kupanua shughuli zake nje ya Afrika Mashariki

 

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba (katikati) akifurahia jambo wakati wa majadiliano na timu ya Taasisi ya Trade Mark East Afrika -TMEA (hawamo pichani) kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya TradeMark East Afrika (TMEA) Bw. David Beer na kulia ni aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TMEA Bw. Frank Matsaert ambaye amemaliza muda wake.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Emmanuel Tutuba akizungumza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Timu ya Taasisi ya TradeMark East Afrika (TMEA) jijini Dar es Salaam. (kulia) na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango (kushoto) timu ya Taasisi ya Trade Mark East Afrika -TMEA
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Tutuba (katikati), akiwa katika picha ya Pamoja na Timu ya Taasisi ya Trade Mark East Afrika -TMEA na baadhi ya viongozi na Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam. kulia ni aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya TradeMark East Afrika (TMEA) Bw. Frank Matsaert, Mkurugenzi Mkazi – TMEA Bi.Monica Hangi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya TradeMark East Afrika (TMEA) Bw. David Beer. Kushoto ni Meneja Mkazi wa Programu – TMEA Bw. Elibariki Shammy, Mchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Muksini Mkumba na Kamishna Mshaidizi Idara ya Madeni Bw. Nuru Ndile.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...