*Awaomba Watanzania kukemea nyufa hizo ,asisitiza Umoja,mshikamano


Na Said Mwishehe, Michuzi Blog

WAZIRI  Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema nyufa za ukabila,udini ambazo mwaka 1995, Mwalimu Nyerere alizungumzia na kuzikeme nyufa hizo bado hazijazibwa kwa sababu ya kuendelea kwa  mambo ya ukabila, udini na ukanda kwenye jamii ya Watanzania.

Akizungumza leo Septemba 20,2022 akiwa mgeni rasmi kwenye Kongamano lilioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation kwa lengo la kutathimini miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo ,Jaji Warioba ameeleza licha ya Mwalimu Nyerere enzi za Uhai wake kukemea nyufa za udini,ukabila na ukanda bado hadi sasa nyufa hizo zimeendelea kuwepo ,hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kukemea hali hiyo.

Jaji Warioba amefafanua kwamba ukabila unaanza kuzungumzwa na hasa katika siasa na kuongeza hakuna kiongozi siku hizi ambaye atagombea asijihusishe na ukabila, mara nyingi wanakimbilia ukabila, ndiyo msingi wa kihezo cha kuchaguliwa.

"Ufa huu umezidi kupanuka, jambo ambalo ni hatari kwa umoja wa kitaifa, niwaombe Watanzania kutafakari jambo hilo na kuona namna ya kuziba ufa uliopo.Sasa tunataka uchifu urudi na  kila chifu akianza kuleta maadili ya kabila lake, hali itakuwaje.Ni wajibu wetu kwa Umoja wetu tutafakari hili na kuona namna ya kuziba nyufa hizi ambazo Mwalimu Nyerere alizikemea," amesisitiza Jaji Warioba.

Akizungumza zaidi kwenye mdahalo huo Jaji Warioba amesema  ukanda nao unazungumzwa hasa kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo linapanua ufa huo na kuhatarisha umoja wa kitaifa.

Ameongeza kuwa  ukanda unazungumzwa sana kwenye mitandao na kwamba  ukizungumzia Muungano yanajitokeza mambo ya ukanda; kwamba Wazanzibari ni bora kuliko wa Bara au wa Bara ni bora sana kuliko Wazanzibari.

Amebainisha nyufa hizo zinajitokeza zaidi kwa wanasiasa, wananchi wenyewe wana woga wa mambo hayo, ndiyo maana wanafanya shughuli zao bila woga wowote.

Kwa upande wa  udini amesema nao upo hasa kwa viongozi wa kisiasa ambao wamekuwa wakitumia nyumba za ibada kama majukwaa ya kisiasa, jambo ambalo sio zuri kama alivyoonya Mwalimu Nyerere.

Jaji Warioba amesema siku hizi viongozi wanakwenda kwenye ibada kama viongozi, sio kama waumini na mara nyingi wanataka wapewe nafasi ya kuzungumza na mambo yanayozungumzwa hayaendani na somo la siku hiyo.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Christina Mndeme ametumia mdahalo huo kuwataka wanasiasa kutofautisha siasa na mambo mengine ya kijamii na kidini hususan wanaotumia nyumba za ibada na matukio ya kijamii kufanya siasa.

" Lazima wanasiasa tuweke mazingira mazuri ya kutofautisha ni wakati gani wa kufanya siasa na wakati gani wa kufanya dini au kushiriki shughuli za kijamii ili tuwe tunatengenisha shughuli za kisiasa na mambo mengine ili shughuli zote ambazo ni tofauti na siasa zifanyike Kwa mujibu wa kanuni na taratibu zake,"amesema Mndeme 

Ametumia nafasi hiyo kuwataka wanasiasa kuacha tofauti zao na kuhakikisha wote kwa ujumla wao wanadumisha amani, umoja na mshikamano kwa maslahi mapana ya Taifa la Tanzania.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku pamoja na mambo mengine amesema Baba wa Taifa alipoanzisha taasisi hiyo baada ya kutakari kwa muda aliamua isimamie maeneo matatu ambayo ni amani, Umoja na maendeleo ya watu wote kwa maslahi yao wenyewe yanayotokana na shughuli zao za kila siku.
Waziri Mkuu Mstaafu,Joseph Waryoba akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba 20,2022  kwenye kongamano lilioandaliwa na Mwalimu Nyerere Foundation katika kukuza amani na maendeleo kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Demokrasia na Usaidizi wa Uchaguzi (IDEA).
Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Warioba( wa tatu kushoto) akifuatilia kwa makini mijadala mbalimbali wakati wa kongamano lilioandaliwa na Mwalimu Nyerere Foundation jijini Dar es Salaam leo Septemba 20,2022
Sheikh Mussa Kundecha akitoa maoni yake wakati wa mdahalo huo ambao amesema ni vema wadau mbalimbali wakawa wa kweli kwa kueleza ukweli wa mambo ambao utasaidia kuweka mambo sawa kwa maendeleo ya Watanzania wote.
Mwenyekiti wa Mwalimu Nyerere Foundation Joseph Butiku akifuatilia mijadala mbalimbali wakati wa Konga hilo

 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...