Na Abdullatif Yunus - MichuziTv Kagera
Taasisi ya Jamii mpya Bukoba Manispaa wameanza Maandalizi kuelekea Wiki ya Vijana itakayoambatana na Shughuli ya Kitaifa ya Uzimaji Mwenge Mkoani Kagera.
Katika Kuelekea Wiki ya Vijana Mwezi ujao ambapo huwa Ni kilele cha Mbio za Mwenge, Tayari Wanajamii mpya Bukoba Manispaa wameanza Shughuli mbalimbali za Kijamii na kuhamasisha Wananchi Kujitokeza kwenye kilele cha mbio za Mwenge ambapo Mkoa Kagera ndio wenye dhamana ya kuzima Mwenge huo.
Miongoni mwa Shughuli zilizofanyika Jumapili hii ya Septemba 18 Ni pamoja na Shughuli za Usafi Eneo la Mwalo wa Kalobera katika Kata ya Bakoba, Shughuli zilizoambatana na Utoaji wa Elimu juu Ugonjwa wa UKIMWI na Matumizi sahihi ya Kondomu kwa jamii ya Wavuvi.
Taasisi hii iliyosambaa maeneo mbalimbali Nchini, Yenye lengo la kusemea kazi nzuri zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kupitia Kampeini yake maarufu "Mama yangu, Nchi yangu" hivyo kwa Bukoba Manispaa Manispaa tayari harakati hizo zimeanza lengo likiwa nikuufahamisha umma Yale yote yanatekelezwa na Mhe. Rais Samia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...