
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma wakiteta jambo kwenye basi la mwendo haraka na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dk.Edwin Mhede (Mwenye kofia)


Katibu Mkuu wa Nchi Ofisi ya Rais Serikali Mitaa na Tawala za Mikoa (OR-TAMISEMI) Profesa Riziki Shemdoe akizungumza kuhusiana utendaji na ziara ya Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kutembelea Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dk.Edwin Mhede akizungumza kuhusiana na utoaji wa huduma wa mabasi yaendayo haraka kwa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma ilipotembelea jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma wakiwa na Mwenyekiti wakifurahi na tiketi katika kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka Kimara.
*Waziri Bashungwa atangaza neema ya mabasi 177 ya kutoa usafiri DAR.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeitaka Serikali kufanya upembuzi yakinifu ya mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT) kwa mkoa Dar es Salaam kuongeza mtandao wa barabara katika kufika sehemu nyingi.
Upembuzi miundombonu ya mradi barabara yaendayo haraka huo ulifanyika mwaka 2004 ambapo kwa wakati huo ndio mahitaji lakini kwa sasa idadi ya watu kubwa ambao wanahitaji kufikiwa huduma ya mabasi yaendayo haraka.
Hayo amesema Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jerry Slaa wakati Kamati hiyo ilipotembelea Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti huyo amesema huduma hiyo katika awamu zingine kwa Barabara ya Kilwa kuishia Vikindu , Barabara ya Bagayo iishie Ekelege na Barabara ya Pugu iishie Pugu na kuhudimia Kisarawe na Chanika.
Kamati hiyo imepongeza Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa kazi wanayofanya ya kuweka mifumo madhubuti ya ukusaji wa mapato na kuongeza kuwa Fedha inayokusanywa na DART iko salama.
Silaa amepongeza DART kwa kutumia mifumo ya TEHAMA katika utoaji huduma na kuwezesha mapato kuongezeka kutoka Sh.bilioni 25 hadi sh.bilioni 36 kwa mwaka wa fedha 2021/22.
Pia amesema kuweka mpango wa kufikisha huduma katika Mikoa mingine kama Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya.
Kwa upande wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba wa kununuliwa kwa Mabasi mapya 177 ya Wakala wa Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es Salaam.
Bashungwa ameeleza ongezeko la mabasi hayo litawezesha DART kuongeza huduma kwa wananchi kutoka kuhudumia abiria 200,000 hadi kufikia 500,000 kwa siku katika vituo vyote vilivyopo sasa Dar es salaam.
"Mabasi ya mwendokasi yamepunguza kwa asilimia kubwa msongamano wa magari katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuwawezesha wananchi kutumia muda mwingi kwenye kufanya kazi za uzalishaji pia kuwawezesha wanafunzi kufika mashuleni mapema bila adha kubwa za foleni," amesema Mhe.Bashungwa.
Aidha, Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe kusimamia kikamilifu DART kufanya usanifu kwa haraka katika maeneo ambayo yapo pembezoni ili kuweka mpango wa kufikisha huduma ya Mabasi ya Mwendokasi, kama maeneo ya Vikindu, Kigambo, ukonga na Chanika.
Waziri huyo amesema dhamira ya serikali ni kuongeza mtandao wa barabara za mwendo wa Haraka kwa kufikisha huduma ya mabasi katika maeneo pembezoni yenye watu wengi na kuboresha huduma katika maeneo ambayo yana huduma za mabasi ya mwendokasi.
Bashungwa amempongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupitisha muundo mpya wa kitaasisi wa Wakala huo ili kuwawezesha kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi wa Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) Dk.Edwin Mhede amesema mchakato wa kadi punde zitaanza kutumika.
Amesema maelekezo yaliyotolewa na kamati watafanyia kazi katika kuendelea kutoa huduma kwa wananchi katika usafirishaji na kukuza uchumi wa nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...