Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akizungumza mara baada kupokea maelekezo ya Kamati kuhusiana Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Seleman Kakoso akizungumza katika kikao cha kamati hiyo na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) , jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Msanifu wa Majengo Daud Kondoro akizungumza kuhusiana na utendaji wa TBA katika kikao cha Kamati ya Bunge, jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu katika kikao na TBA , jijini Dodoma.

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imepokea, kujadili na kushauri taarifa ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). 

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi wa TBA, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Suleiman Kakoso ametoa pongezi na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na Wakala huo.

Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa miradi yenu, ila hakikisheni mnaweka mikakati inayotekelezeka kwani uwekezaji kwenye ujenzi wa nyumba unakuwa wa kubadilika kila siku hivyo mnatakiwa muende sambamba na mabadiliko hayo ili kuweza kupata wateja ndani na nje ya nchi, amesema Kakoso.

Aidha, Mhe. Kakoso ameitaka TBA kuhakikisha inaendelea kubuni miradi mbalimbali katika maeneo ambayo wanamiliki ili kulinda maeneo yao pamoja na kusambaza huduma kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesisitiza TBA kuendelea kuwa wabunifu kwa kuhakikisha inaendelea kujenga na kukarabati nyumba na majengo ya Serikali ili kuongeza ubora wa makazi kwa viongozi na watumishi wa umma.

Waziri Mbarawa ameitaja miradi mikubwa ya kitaifa ambayo imetekelezwa na TBA kuwa ni ujenzi wa nyumba za makazi za Magomeni Kota, jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sekou-Toure Mwanza, jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Ujenzi wa makazi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Usimamizi wa mradi wa ujenzi wa Ikulu Chamwino Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...