WATAALAMU wa magonjwa ya moyo ya watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa nchini Saudi Arabia ambao ni moja ya mradi wa Afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza watafanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto kuanzia tarehe 10 hadi 14/10/2022.

Tarehe 17/10/2022 hadi 21/10/2022 wataalamu wetu watakuwa na kambi ya  upasuaji wa moyo na wenzao kutoka  Shirika la Kimataifa la Mending Kids la nchini Marekani na tarehe 29/10/2022 hadi 13/11/2022 kutakuwa na kambi ya upasuaji wa moyo kwa kushirikiana na mtaalamu kutoka nchini  Ujerumani.

Tunawaomba wazazi na madaktari wenye watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo; matundu, mishipa ya damu ya moyo kutokuwa katika mpangilio wake (ASD for device closure, PDA for device closure, VSD, & Pulmonary valvular stenosis) wawalete katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi au upasuaji kwa wale itakaohitajika.

Aidha tunawaomba wananchi kuendelea kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa. Mgonjwa mmoja anayefanyiwa upasuaji wa moyo anatumia kati ya chupa sita hadi saba za damu. Hivyo basi mahitaji ya damu ni makubwa kwa mgonjwa anayefanyiwa upasuaji wa Moyo.

 

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa namba 0757843481 Dkt. Jackline Olesyaiti, 0744479506 Dkt. Jimmy France na 0782042019 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...