-Hatua hiyo ni sehemu ya kusherekea miaka 90 ya kampuni hiyo kubwa duniani
Kampuni Eureka Trading Tanzania imezindua bidhaa tano mpya za wine, hatua ambayo inaipa nguvu zaidi kampuni hiyo yenye miaka 90 kwenye soko la dunia.
Eureka Trading ni sehemu ya kampuni mama ya Oxenham yenye makao yake nchini Mauritius ambayo ilianzishwa mwaka 1932 ikitambulika kwa bidhaa zenye viwango vya kimataifa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa hizo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Alan Oxenham alisema kwa kutumia uzoefu wa kampuni hiyo nchini Mauritius, wamejizatiti kutumia ubora huo kuleta ladha tofauti kwenye soko la Tanzania.
“Nina furaha kuwa sehemu ya familia hii kubwa na kutambulisha bidhaa hizi kwa jina la Eureka Trading Tanzania, bidhaa zetu hizi zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa nchini Mauritius na tunafuraha kuzileta hapa nchini,” alisema.
Bidhaa hizo ni Frizante grape fruit, Frizante lime, Oxano semi sweet, Avino sweet red 18% vol and Oxenham old port zenye sifa tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya mteja ikiwamo ladha pamoja na kiasi cha kilevi.
“Bidhaa yetu ya Frizante Grape Fruit ni laini na yenye ladha ya rose na yenye harufu nzuri sana.Ni kinywaji kizuri kwa kunywa kabla ya kula lakini pia kinafaa kwa matumizi mengine.Ni kinywaji mahususi kwaajili ya msimu wa joto ili kukufanya kujisikia murua,” alisema.
Frizante lime ni kinywaji chenye povu (bubble) na chenye harufu nzuri na yenye kuvutia.Ni kinywaji kinachofaa kwa matumizi ya aina zote na wakati wowote.
Kuhusu Oxano Semi Sweet, Alan Oxenham anasema “Kina rangi nzuri ya dhahabu na chenye harufu nzuri sana.Kimetengenezwa kwa viungo vyenye ladha ya matunda na mimea.”
Avion Sweet red 18% ni kinywaji chenye ladha tamu na muonekano wa thamani na harufu nzuri wakati Oxenham Old Port imetengenezwa maalumu kwaajili ya kuupa mwili joto wakati wa baridi.
Bidhaa hizi kwa sasa zinapatikana jijini Dar es Salaam lakini zitasambazwa kwenye Mikoa mingine siku za hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...