Na Mwandishi wetu, Babati


MDAU maarufu wa maendeleo wa Mji Babati Mkoani Manyara, Emmanuel John Khambay amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Babati Mjini.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Babati Mjini Hamisi Tsaxara amesema Khambay amewashinda wagombea wenzake wawili waliokuwa wakigombea nafasi hiyo.

Tsaxara amesema Khambay ameshinda nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Babati Mjini kwa kupata kura 112.

Amesema nafasi ya pili imeshikwa na Thomas Ng'ayda Samo aliyepata kura 49 na Nada Siasi Oye alishika nafasi ya tatu kwa 25.

"Nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ameshinda Wilhelmon Mayo aliyepata kura 128
na Neema Ramadhani akapata kura 51," amesema Tsaxara.

Amesema nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu CCM Mkoa ameshinda Boniface Mwita kwa kupata kura 93 na Frank Lobulu akapata kura 77.

Amesema nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa wazazi Mkoa ameshinda Ismail Iddy Mshana kwa kupata kura 146, Abubakari Ama kura 21 na Muhamad Husein 10.

Akizungumza baada ya kushinda nafasi hiyo Khambay amewashukuru wajumbe hao kwa kumpa kura nyingi hadi akashinda nafasi hiyo.

"Uchaguzi umemalizika hivyo sisi kama wazazi tuhakikishe tunajipanga tunatimiza wajibu wetu ikiwemo kubuni miradi ya maendeleo ya jumuiya ya wazazi,"
amesema Khambay.

 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...