Makamu Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Kinana ameishauri
Kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL) kujiendesha na kuanza kufikiri
kibiashara ikiwemo kuomba dhamana za serikali Ili kukopa fedha na
kununua meli mpya ili kukidhi mahitaji ya huduma za usafiri na
usafirishaji katika ziwa Tanganyika.
Amesema hayo wakati
alipotembelea na kukagua ukarabati wa meli ya MV. Sangara mjini
inagharimu shilingi bilioni 8.4 ameshauri ni muhimu kampuni hiyo
ifikirie kibiashara zaidi. Aidha Kinana ameipongeza serikali ya CCM
Awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kuendelea na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Hiyo ni baada
ya kuambiwa kuwa kama meli hiyo ambayo ni ya mafuta ikikamilika bado
mahitaji ya huduma za meli kwenye ziwa Tanganyika ni makubwa na kwamba
zinahitajika meli nyingine tatu.
“Sikilizeni ndugu zangu
msisubiri hela kutoka bajeti ya serikali, ombeni dhamana ya serikali
mkakope mnunue meli mpya.. pesa za namna hiyo ziko nyingi duniani.”
alisema Kinana.
Kinana pia alipata nafasi ya kutembelea meli
kongwe kabisa duniani ya MV Liemba ambayo nayo ipo kwenye mpango wa
kukarabatiwa kwa kiwango kikubwa na serikali katika mwaka huu wa fedha
2022/2023. Meli hiyo ya mv Liemba ina umri wa zaidi ya miaka 100 na
imeingia kwenye orodha ya urithi wa dunia chini ya UNESCO.
“Ikikamilika mniambie nitakuja na mwenezi kusafiri nayo.” alisema Kinana.” Amesema Kinana
Kinana
ambaye ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na
Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka ameanza ziara yake ya siku tano katika
mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita na Mwanza
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndg Abdulrahman
Kinana akikagua meli ya mafuta MT.Sangara ya Kampuni ya huduma za meli
nchini (MSCL) iliyokuwa inafanya kazi Katika ziwa Tanganyika mkoani
Kigoma kabla ya kusimama Kwa ukarabati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...