Na Mwandishi wetu, Simanjiro

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Manyara Kiria Laizer ambaye amepitishwa na Halmashauri kuu ya CCM Taifa, kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Simanjiro amekishukuru chama hicho kwa kumuamini.

Juzi Halmashauri kuu ya CCM Taifa ilirudisha majina matatu ya Kiria Laizer, Anna Shinini na Haiyo Mamasita, kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Simanjiro

Kiria amesema anakishukuru chama kwa maamuzi hayo na anatoa ahadi kuwa nafasi aliyoiomba ataitendea haki endapo atapewa ridhaa ya kuwa Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo.

"Tutashirikiana pamoja wanachama, chama na Serikali kwa ujumla kufanikisha maendeleo ya wananchi yanapatikana na kuhakikisha umoja na mshikamano unakuwepo,” amesema Laizer.

Mwanachama wa CCM kutoka Kata ya Loiborsiret ambaye pia ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Orkiringo, Mosses Sanjiro amesema Kiria anafaa kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Simanjiro kwani hana siasa za makundi.

"Kiria ndiyo mtu sahihi wa kuiongoza CCM Simanjiro kwa sasa kwani miaka yake 10 ya kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Simanjiro tuliona alivyokuwa hana makundi hivyo apewe nafasi," amesema Sanjiro.

Mwanachana mwingine Raphael Siria amesema Kiria ni kijana msomi na anailewa simanjiro vizuri sana hivyo anaona anatosha kuwavusha na kuitoa simanjiro kwenye siasa ya makundi.

Siria amesema siasa ya makundi inaharibu kwani imefika mahali baadhi ya mashina Simanjiro yameshidwa kumaliza uchaguzi kwa kuingiliwa na wilaya ni aibu na aibu kubwa.

Katibu wa CCM wilaya ya Simanjiro, Amos Shimba amesema uchaguzi wa kugombea nafasi mbalimbali za wilaya hiyo unatarajiwa kufanyika Oktoba 2 mwaka huu kuanzia saa 4 asubuhi.

Shimba ametaja baadhi ya nafasi zitakazogombewa ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya, katibu mwenezi wa wilaya, wajumbe watatu wa mkutano mkuu wa Taifa na wajumbe wa mkoa na wilaya.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...